Shabiki wa Simba auawa kisa tobo la Banda

Shabiki wa Simba auawa kisa tobo la Banda

Kukaja Kununu

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2017
Posts
1,077
Reaction score
1,208
Shabiki wa simba anaejulikana kwa jina la Agustino Mwangosi kutoka kijiji cha kingiri kata ya Ipinda wilayani Kyela, auwawa na shabiki wa yanga (Jina Kapuni) kisa ikiwa ni majibizano ya mchezaji wa Simba Peter Banda kupigwa mpira uliopita katikati ya miguu (TOBO).

Akizungumza na kyela fm katika kipindi cha KONA YA MICHEZO diwani wa kata ya Ipinda Eliah Mwaipetania, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akielezea kuwa marehemu alikuwa katika hali ya majibizano ya kishabiki na mtuhumiwa walipokuwa wakitazama mchezo wa Simba Vs Pamba katika Hatua ya robo fainali ya kombe la ASFC.

Katika majibizano hayo ilionyesha mtuhumiwa kutopendezwa na majibu ya marehemu, ndipo mtuhumiwa akaondoka eneo la tukio (KIBANDA UMIZA) na kuamua kumvizia marehemu wakati akirudi na kumuua kwa kumpiga na gogo sehemu mbalimbali za mwili na kupelekea umauti wake.

Diwani Mwaipetania amesema mwili wa marehemu umezikwa jumapili 15/05/2022 na hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya mtuhumiwa. Diwani amewataka mashabiki wa mpira kuacha ushabiki wa hovyo na mpaka kupelekea kuuana.

 
Mwaka huu tutawapiga kotekote uwanjani na nje ya uwanja mpaka makolo mkae sawa, humu ingekuwa tunaonana ningempiga makwenzi kila siku kolo Scars
ni kwa kuwa upo huru uraiani, lakini mwenzako atakuwa gerezani kwa kipindi kisichojulikana akisubiri kunyongwa mpaka kufa
 
Kwa nini mashabiki wa utopolo ni wagomvi hivi? Kuna shabaki wa Simba Tabora alitolewaga jicho na shabiki wa utopolo kisa ushabiki tu. Mi sipendagi kubishana kabisa na utopolo wako very unstable.
 
Kwa nini mashabiki wa utopolo ni wagomvi hivi? Kuna shabaki wa Simba Tabora alitolewaga jicho na shabiki wa utopolo kisa ushabiki tu. Mi sipendagi kubishana kabisa na utopolo wako very unstable.
Na mimi nasemwa mpigwe tu
 
Kama sio mvumilivu mabishano ya mpira,kabila,dini hivyo vitu vya kuepuka kabisa kuna wengine hawana uvumilivu kabisa .
Kama unajijua hauna uvumilivu achana na hivi vitu maana kuna watu wana matani mabaya sana unataniwa mpaka unahisi mifupa inatetemeka.
Ebu fikiria umevaa zako jezi ya njano halafu mtu anakuita kabwili au mama jeni😄😄
 
Back
Top Bottom