Shaffi Dauda kuwa makini

Shaffi Dauda kuwa makini

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nimesikia wazungu wamekutafuta uwape details kuhusu Mbwana Samatta. Na wewe ukaahidi utawaambia kuwa tunao wachezaji aina ya Samatta wengi.

Sina tatizo kabisa na details za Samatta. Sina shida na kuwatangaza vijana wote wenye uwezo kama wa Samata ambao naamini wapo. Tatizo langu, ni je wana thamani ya Samatta?

Maana tuna tamaduni mbaya sana ambazo zimeathiri sana tabia, mitizamo, na maono yetu juu ya mambo muhimu kwenye maisha. Tuna wachezaji wasiojituma, walevi, malaya na wasio na maono.

Wengi wakishadajiliwa Yanga na Simba au Azam wanaona wamefika. Hawajipi muda wa ziada wa mazoezi, hawajitunzi afya zao, kwa ujumla hawana nidhamu.

Watu kama hao, ukiwatambulisha kwa wazungu, wakaenda na tabia za uswahili Swahili, watakuwa kikwazo kwa vijana wengine kama Mbwana Samatta watakaotokea baadae. Kwa sasa sijawaona. Wengi wana ujinga ujinga mwingi tu. Wanacheza kama vile ni mastar wa dunia, kumbe wako Yanga tu au Simba.

Inabidi kuwe na jitihada za maksudi za kubadilisha tamaduni zetu kama kutothamini kazi, kutojali muda, kupenda starehe kuliko kazi, kusema uongo, kutokuwa wavumilivu (tunakata tamaa mapema) tofauti na wazungu utaona zimebaki dakika 2 ila wanaforce hadi wanapata goli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yuko timu gani huko?
Yupo wa kwangu anacheza Afrika Kusini. Ana nidhamu ya hali ya juu. Imagine ameenda hana anayemjua na ameweza kuishi miaka 4 bila kukata tamaa na kujiunga na makundi ya kihuni. Focus yake ni soka tu.
 
Back
Top Bottom