Shaffi Dauda ni mtu wa fitna sana ili afanikishe dili zake

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Moja ya watu wenye uchu mbaya wa pesa kupitia vilabu vikubwa ni huyu mtu anaitwa Dauda. Ni mmoja wa virusi vikali sana anayetafuta kwa njia zote za fitna kupata fursa pale Klub ya Simba ili apige dili zake.

Kama kuna watu wanaochangia kuvuruga sana maendeleo ya mpira kwa ngazi za vilabu, mmoja wapo ni hili gwiji la fitna zinazopangwa kwa akili na watu wenye akili tu wanaweza kugundua njama zote.

Hivi sasa ana kampeni ya kutaka CEO aondoke kwa kigezo cha Simba kupoteza mechi na kutomfunga Yanga. Analalamika kwanini wafukuzwe makocha tu wakati kiongozi yupo na hajatimiza malengo. Hata hivyo huyu anayejinasibu ni mchambuzi wa soka hajui kuwa hata Ulaya makocha hufukuzwa lakini viongozi wakiendelea na majukumu yao.

Mijitu yenye roho mbaya kama huyu jamaa, iko tayari kufanya lolote ili ipate upenyo wa kuanzisha hoja kama hizi. Usije shangaa hata usajili unaofanywa, kuna mkono wa jitu kama hili. Na linafanya hivi likiwa na nia ovu ambayo itatekelezwa baadaye sana.

Nachukizwa sana na maoni ya huyu jamaa dhidi ya Simba kwani huwa hayana lengo la kujenga ila kuvuruga na katika vurugu hizi watu kama yeye wanajipatia fursa.
 
Dauda ni mjanja mjanja, ili mradi yake yaende.
Ukiona anaongelea jambo ana manufaa nalo.
 
Shaffih anapanga line up ya simba?

Shaffih ndio anamuambia kyombo kua akose magoli?

You guys,Why don't you want to appreciate the performance of Azam yesterday?

Nyie ni kina nani msifungwe?

Mbona kila mkifungwa mnamtafuta mchawi.
Shafii ametoa maoni babra asepe lakini tujiulize babra ndio anamwambia kayombo akose magoli ya wazi kiasi kile? Au babra kosa lake kumleta kayombo ambae anakosa magoli ya wazi?
 
Mlikuwa mnashabikia Nabi afukuzwe hamkujuwa hizo ni hila za watu?

Haya Sasa bundi yupo Msimbazi pambaneni na hali yenu, Mtibwa wanakuja kupiga kwenye mshono hapo ndio ticket ya Mgunda kurudi Tanga na raha leo.
 
Unachukia maoni ya shaffi dauda dhidi
Ya

Unachukia maoni ya shaffi dauda kuisema simba lakini wakati huo huo unayapenda maoni ya jemedari said anapoisema yanga
 
Mlikuwa mnashabikia Nabi afukuzwe hamkujuwa hizo ni hila za watu?

Haya Sasa bundi yupo Msimbazi pambaneni na hali yenu, Mtibwa wanakuja kupiga kwenye mshono hapo ndio ticket ya Mgunda kurudi Tanga na raha leo.
Na ikitokea kupigwa kesho ataondoka na msaidizi wake.
 
Huyo mizizi yake ilishakatwa... hana madhara, ni boya fulani linaelea ila lina tundu, litazama muda si mrefu...
Pia aache kuwanyonya madogo anaodai kuwasapoti... jamaa ninkupe fulani hivi nyonya damu, ceo wa simba ana akili kubwa sana hivyo huyi boya hamuwezi kabisa...
 
Unachukia maoni ya shaffi dauda dhidi

Ya



Unachukia maoni ya shaffi dauda kuisema simba lakini wakati huo huo unayapenda maoni ya jemedari said anapoisema yanga
Shaffi ana kinyongo na CEO kwani amenyimwa fursa ya kupiga dili,Jemedari anaweza kuwa anawaambia ukweli mchungu ambao hamtaki kuusikia
 
Ametengenezwa na taasisi yake UBINAFSI na kuwagandamiza Wengine kwa manufaa Binafsi.
 
Edo mwembe na yule mchambuzi wa wasafi mwenye kipara wanabusara sana hawa jamaa ila ayo mengine njaaa tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…