Shaffih Dauda afunguka kuhusu kukamatwa kwake na TAKUKURU

Shaffih Dauda afunguka kuhusu kukamatwa kwake na TAKUKURU

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253


Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU kwa mwenyekiti wa chama cha mpira Dar es Salaam DRFA Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza

Taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kukamatwa kwa watu hao zinadai ni viashiria vya rushwa na kuhusishwa na kampeni za chini kwa chini za uchaguzi Mkuu wa TFF, hivyo TAKUKURU ikawakamata kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa kadhaa kabala ya kuwaachia kwa dhamana.

Baada ya kurejea Dar es Salaam akitokea Mwanza Shaffih Dauda alipokuwa amekwenda na viongozi wa DRFA kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup kupitia Clouds FM ameeleza tukio la kukamatwa kwao lilivyokuwa ambalo linadaiwa kulenga kuwachafua katika uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Nimehojiwa na TAKUKURU nikiwa Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup ambayo inaweza kuanza Mwezi wa 9, nilichogundua ni siasa za uchaguzi wa TFF, nilikutana na viongozi wa mpira Mwanza kwa ajili ya mipango ya Ndondo Cup Nilikua na viongozi wa DRFA tulioanzisha nao Ndondo Dar”>>> Shaffih Dauda

“Viongozi wa DRFA walikuwepo Mwanza kuwaeleza uzoefu viongozi Mwanza kabla hawajafanya na wao mwaka huu, baadhi ya watu na mawazo yao walitoa taarifa za uongo na kufanya mipango ya hovyo wakijua nafanya mipango ya uchaguzi, sigombei TFF kutaka cheo, nagombea kuleta mabadiliko kwenye soka, ndio maana napambana kupeleka Ndondo Cup kila sehemu” >>> Shaffih Dauda

Kwa Hisani ya Salehe Jembe
 
sigombei TFF kutaka cheo, nagombea kuleta mabadiliko kwenye soka, ndio maana napambana kupeleka Ndondo Cup kila sehemu” >>> Shaffih Dauda
Heeeeee kama soka letu litabadilishwa kwa ndondo cup, basi sawa.........., huyu jamaa huwa namkubali sana kwenye mpira, ana exposure kubwa sana, katembelea clubs kubwa duniani na hata kufanya mahojiano na magwiji wakubwa wa soka, leo anagombea uongozi afu anasema ili kukuza soka la Tanzania tuwe na mashindano ya ndondo cup, si utahira huu!!!!!!!! Hivi huko ulaya anakotembea kila siku amewahi kukuta hiyo ndondo cup??
 
Back
Top Bottom