Shaffih Dauda mfukuze kazi Baraka Mbolembole

Me nadhani hata yeye atakua mshabiki kama ulivyokua wewe! Huna haja ya kumuharibia mwezio kibarua chake! kama anaisema simba kila mara na wewe hupendi basi usisome makala zake! Soma hizo blogs nyingine ulizozitaja
Mbona hata huyo shafii ni kusema Yanga vibaya kwahyo naye vipi?
 
Mimi ni mmojawapo wa wasiokubaliana na uamuzi wa mlalamikiwa kuandika makala dhidi ya Simba pekee. Siridhiki na makala za waandishi wengi, wakiwamo hao waliosifiwa na mtoa mada, kwa sababu nao wanalazimisha mawazo yao kwetu badala ya kutupa taarifa. Ningekubaliana nao kama blogu ama vyombo wanavyoandikia vingesajiliwa na kuasisiwa mahsusi kuwa ni vya taaluma, siyo kuhabarisha. Lakini naheshimu makala za wote hao (akiwamo mlalamikiwa) kwa sababu kwanza wanajitofautisha na waandishi wengine na pili wanatumia haki yao ya kidemokrasia ya kutoa mawazo yao. Wanatumia uandishi wenye ladha tofauti na iliyozoeleka. Nilidhani njia sahihi ya kupambana na mlalamikiwa ni kuja na makala mbadala, labda Mboni ya Nne, itayokuwa angalau ikikosoa kasoro zake au vinginevyo kuisifia Simba kama siyo kuinanga Yanga (au Azam?).
Tukumbuke kuwa miongoni mwa madhumuni ya uhuru wa habari ni kupata mawazo tofauti ya jambo hilohilo moja kutoka kwa watu tofauti wenye mtizamo tofauti. Ndiyo raha ya demokrasia ambayo wengi wetu ni wahubiri wake wazuri. Hii ya kukerwa na mawazo huru ya wengine ndiyo adha ya demokrasia hiyohiyo. Dawa si kumfungia wala kumfukuza. Ukimfungia watakuja wengine kama au zaidi ya yeye. Dawa ni kuzowea na kustahamili adha za namna hiyo. Ila nayo ina faida yake ambayo wote wanaoipenda Simba wanatakiwa waione. Nayo ni kujua adui wako anafikiriaje juu yako. Hilo litakuwezesha kujipanga vizuri dhidi yake, kuliko kutumia ukosoaji binafsi (self criticism) ambao ni adimu sana kuiangalia Simba kwa jicho la tatu. Au kupitia kwa uongozi na waandishi wanaoushabikia ambao wanaelekea kuwaaminisha wanachama na wapenzi kwamba una Simba ya Utopia.
Mwandishi mmoja alipata kusema 'sikubaliani na mawazo yako, lakini nitapigana hadi kufa kutetea haki yako ya kuyatoa.' Tunatakiwa tuwe kama yeye, la sivyo neno demokrasia lifutwe kwenye tunu za Taifa letu.
 
Hongera mleta mada kwa hoja na ushahidi dhahiri dhidi ya Mbolembole. Ipo dhana kuwa mwandishi huyu ni mpenzi wa Simba aliyeathirika na siasa za kutafuta uongozi ndani ya timu hiyo kwa hiyo ana chuki kuu ambayo bahati mbaya ameshindwa kuitafutia dawa. Badala yake amechanganya chuki na kazi. Kwa kuwa anataka kuwakomoa baadhi ya watu lakini anashindwa kujua kuwa hawatendei haki wengine ambao hawana upande lakini kubwa kuitendea haki fani yake inayomtaka kuwa objective na kuepuka biasness.

Kusema kweli anasikitisha sana maana chuki inaonekana dhahiri ni kama anashindana na watu fulani hivi ndani ya Simba. Siamini kama anafanya kazi kwa faida ya Yanga, ila ana chuki na Simba japo hajatumwa na Yanga.
Aisee namfahamu huyu bwana, maelezo yako ni sahihi kwa 99%. Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba anamchukia sn Kaburu, Hans Poppe na friends of Simba wote. Yeye nafkiri alimtaka Wambura wakati ule
 
Mimi ni mmojawapo wa wasiokubaliana na uamuzi wa mlalamikiwa kuandika makala dhidi ya Simba pekee. Siridhiki na makala za waandishi wengi, wakiwamo hao waliosifiwa na mtoa mada, kwa sababu nao wanalazimisha mawazo yao kwetu badala ya kutupa taarifa. Ningekubaliana nao kama blogu ama vyombo wanavyoandikia vingesajiliwa na kuasisiwa mahsusi kuwa ni vya taaluma, siyo kuhabarisha. Lakini naheshimu makala za wote hao (akiwamo mlalamikiwa) kwa sababu kwanza wanajitofautisha na waandishi wengine na pili wanatumia haki yao ya kidemokrasia ya kutoa mawazo yao. Wanatumia uandishi wenye ladha tofauti na iliyozoeleka. Nilidhani njia sahihi ya kupambana na mlalamikiwa ni kuja na makala mbadala, labda Mboni ya Nne, itayokuwa angalau ikikosoa kasoro zake au vinginevyo kuisifia Simba kama siyo kuinanga Yanga (au Azam?).
Tukumbuke kuwa miongoni mwa madhumuni ya uhuru wa habari ni kupata mawazo tofauti ya jambo hilohilo moja kutoka kwa watu tofauti wenye mtizamo tofauti. Ndiyo raha ya demokrasia ambayo wengi wetu ni wahubiri wake wazuri. Hii ya kukerwa na mawazo huru ya wengine ndiyo adha ya demokrasia hiyohiyo. Dawa si kumfungia wala kumfukuza. Ukimfungia watakuja wengine kama au zaidi ya yeye. Dawa ni kuzowea na kustahamili adha za namna hiyo. Ila nayo ina faida yake ambayo wote wanaoipenda Simba wanatakiwa waione. Nayo ni kujua adui wako anafikiriaje juu yako. Hilo litakuwezesha kujipanga vizuri dhidi yake, kuliko kutumia ukosoaji binafsi (self criticism) ambao ni adimu sana kuiangalia Simba kwa jicho la tatu. Au kupitia kwa uongozi na waandishi wanaoushabikia ambao wanaelekea kuwaaminisha wanachama na wapenzi kwamba una Simba ya Utopia.
Mwandishi mmoja alipata kusema 'sikubaliani na mawazo yako, lakini nitapigana hadi kufa kutetea haki yako ya kuyatoa.' Tunatakiwa tuwe kama yeye, la sivyo neno demokrasia lifutwe kwenye tunu za Taifa letu.

Well observed!
 
Back
Top Bottom