Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Akiwa katika kipindi cha michezo cha Sports Extra ya Clouds Fm, mchambuzi Shaffih Dauda amesema sababu kuu ya Mukoko kuuzwa na Yanga kwenda TP Mazembe ni kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa Fainali ya FA dhdi ya Simba.
Katika mchezo huo, Mukoko Tonombe alimpiga kiwiko John Bocco na kupewa red card na kusababisha Yanga kupoteza mchezo huo.
Shaffih aliongeza "Ndani ya Yanga kuna wahafidhina walimuona Mukoko kama aliuza mechi, hivyo wakapanga kumuondoa kikosini taratibu"
Haiingii akilini, mchezaji bora wa msimu uliopita eti kushindwa kupata nafasi katika kikosi hiko, Mukoko kaondolewa kimchongo, aliongeza Shaffih.
Je, unamuunga mkono Shaffih au unampinga?