Shaffih Dauda: Mukoko Tonombe kauzwa kwasababu ya red card ya Fainali ya F.A

MCHAMBUZI WA MCHONGO, CHUPLICHUPLI
Akiwa katika kipindi cha michezo cha Sports Extra ya Clouds Fm, mchambuzi Shaffih Dauda amesema sababu kuu ya Mukoko kuuzwa na Yanga kwenda TP Mazembe ni kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa Fainali ya FA dhdi ya Simba.

Katika mchezo huo, Mukoko Tonombe alimpiga kiwiko John Bocco na kupewa red card na kusababisha Yanga kupoteza mchezo huo.

Shaffih aliongeza "Ndani ya Yanga kuna wahafidhina walimuona Mukoko kama aliuza mechi, hivyo wakapanga kumuondoa kikosini taratibu"

Haiingii akilini, mchezaji bora wa msimu uliopita eti kushindwa kupata nafasi katika kikosi hiko, Mukoko kaondolewa kimchongo, aliongeza Shaffih.

Je, unamuunga mkono Shaffih au unampinga?
 
Tukianza na mechi yenyewe ya fainali ya FA pale tabora nani alikua bora kuliko mwingine kati ya simba na Yanga? Jibu ni rahisi sana kwa wakati ule simba alikua bora sana.

Swali lingine je,mukoko asingetoka yanga wangeshinda ile game? Jibu ni ni rahisi tu "labda" ila kwa mtazamo wangu ni "hapana". Kwanini nasema hapana! Ni kwa sababu Simba alikua bora sana kuliko yanga, wengine moyoni wataguna mbona Yanga alimfunga simba kwenye ligi.. Yap ni kweli alimfunga tunajua.. Ila tujikumbushe nyuma kidogo msimu mmoja nyuma zaidi simba hakuwahi kumfunga yanga kwenye ligi ila nusu fainali ya FA alimfunga goli nne moja.. Kwahiyo kwa kigezo cha ubora bado simba wangeshinda tu.

Sasa nije kwenye hoja ya Shaffih dauda kua Wanazi wa yanga wamemuuza mukoko kwenda TP mazembe kisa " aliuuza mechi". Kwanza sijui kama in kweli kauzwa au ni "maneno" tu japo nilimsikia Mbumbuli akisema wamemuuza Mukoko pia kwa kumchukua Ushindi sasa sijajua kwanini bado mukoko yupo jangwani maybe dirisha la usajili Congo bado halijafunguliwa au anamalizia msimu!? Sijui.

Lakini hoja hii japo inaweza kua na ukweli mwingi ndani yake lakini mi naamini Kuna inshu haipo sawa kati ya Yanga na mukoko na nahisi tatizo lilianzia kwenye dirisha kubwa lililopolita coz kipindi Tuisila Kisinda anaondoka yanga na mukoko pia alitakiwa kusepa sema yanga ni kama walikwamisha hilo dili sasa nazani hapo Kuna inshu ilitokea ambayo imepelekea Mukoko kutolewa kafara maana ukirejera lile tukio la red card mashabiki wa yanga walikua upande wa mukoko hakuna aliyemlaumu...

Nipo kwenye group la WhatsApp la yanga makao makuu.. Wadau wote walimtetea mukoko sasa hao wahafidhina ni kina nani kama mashabiki walikua upande wa mukoko?? Anyway huenda hoja yake INA mashiko.. Ngoja tuendelee kunywa mchuzi nyama tutazikuta chini.

#mwananchi mwema [emoji172][emoji169]
Maelezo mengi wakati Hujui hata game ilipigwa uwanja gani? Ilikuwa Lake Tanganyika Kigoma siyo Tabora.
 
Ndio wachambuzi wetu,wenzetu ulaya kazi kama hizi wanafanya wachezaji waliocheza ligi kuu. Huku sijui kigezo gani yani vipindi vyao ni sawa na vile vijiwe vyetu vya mtaani/kahawani.

Tanzania hii mtu aliyekizi kuitwa mchambu Ally Mayai na Kiemba, wengine madeal wanapeana kishkaji,yaani leo Dauda nime mweka kundi moja na Manara.

Sababu za kipuuzi kabisa.
 
kwenye Uelewa wa mchezo wa mpira wa miguu hamna kama shaffih ndo maana kila timu haimpendi !!
Wakati wa dirisha kubwa la usajili, kipindi ambacho Kisinda aliuzwa na Mukoko pia alihitajika na timu mbali mbali ila uongozi wa Yanga ukamchomolea kuondoka. Kama ingekuwa sababu ni ya fainali ya kombe la Azam basi wangeshamuuza kipindi cha dirisha kubwa
 
Tukianza na mechi yenyewe ya fainali ya FA pale tabora nani alikua bora kuliko mwingine kati ya simba na Yanga? Jibu ni rahisi sana kwa wakati ule simba alikua bora sana.

Swali lingine je,mukoko asingetoka yanga wangeshinda ile game? Jibu ni ni rahisi tu "labda" ila kwa mtazamo wangu ni "hapana". Kwanini nasema hapana! Ni kwa sababu Simba alikua bora sana kuliko yanga, wengine moyoni wataguna mbona Yanga alimfunga simba kwenye ligi.. Yap ni kweli alimfunga tunajua.. Ila tujikumbushe nyuma kidogo msimu mmoja nyuma zaidi simba hakuwahi kumfunga yanga kwenye ligi ila nusu fainali ya FA alimfunga goli nne moja.. Kwahiyo kwa kigezo cha ubora bado simba wangeshinda tu.

Sasa nije kwenye hoja ya Shaffih dauda kua Wanazi wa yanga wamemuuza mukoko kwenda TP mazembe kisa " aliuuza mechi". Kwanza sijui kama in kweli kauzwa au ni "maneno" tu japo nilimsikia Mbumbuli akisema wamemuuza Mukoko pia kwa kumchukua Ushindi sasa sijajua kwanini bado mukoko yupo jangwani maybe dirisha la usajili Congo bado halijafunguliwa au anamalizia msimu!? Sijui.

Lakini hoja hii japo inaweza kua na ukweli mwingi ndani yake lakini mi naamini Kuna inshu haipo sawa kati ya Yanga na mukoko na nahisi tatizo lilianzia kwenye dirisha kubwa lililopolita coz kipindi Tuisila Kisinda anaondoka yanga na mukoko pia alitakiwa kusepa sema yanga ni kama walikwamisha hilo dili sasa nazani hapo Kuna inshu ilitokea ambayo imepelekea Mukoko kutolewa kafara maana ukirejera lile tukio la red card mashabiki wa yanga walikua upande wa mukoko hakuna aliyemlaumu...

Nipo kwenye group la WhatsApp la yanga makao makuu.. Wadau wote walimtetea mukoko sasa hao wahafidhina ni kina nani kama mashabiki walikua upande wa mukoko?? Anyway huenda hoja yake INA mashiko.. Ngoja tuendelee kunywa mchuzi nyama tutazikuta chini.

#mwananchi mwema [emoji172][emoji169]
Kazi ya shabiki ni kushangilia tu,ila timu ina wenyewe,wanaamua nani auzwe nani anunuliwe nani abaki,h uko kwenye magroup yenu ya whatspp hata mlie mgaregare haisaidii kuzuia mchezaji kuuzwa
 
Hakuna mchambuzi boya kama Shafii Dauda
kabisa yaani

991DC568-6D7D-4B50-ACD5-328997B88A02.jpeg
 
Mimi nashauri aina hii ya wachambuzi wanao ongea mambo sensitive kama haya, huku wakiwa hawana uthibitisho wowote ule, basi wangepuuzwa tu.
 
Back
Top Bottom