Shaffih Dauda: Taifa Stars inahitaji mtu zaidi ya kocha

Shaffih Dauda: Taifa Stars inahitaji mtu zaidi ya kocha

MFIZIGO

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
374
Reaction score
233
Maneno haya (sijui kama yeye mwenyewe anakumbuka) aliyazungumza Shaffih Dauda January 2010 baada ya stars kushindwa kufuzu AFCON 2010 na World Cup mwaka huo chini ya maximo.
Katika uchambuzi wake ambao mimi nilimuunga mkono 100% kuwa "tatizo siyo kocha kwa taifa stars, tatizo ni MKURUGENZI WA UFUNDI (Expert). Badala ya kutafuta kocha TFF lazima itafute mtu ambaye ni expert kutoka katika nchi zilizo endelea kama vile Argentina au Spain kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa mpira wetu nchi. Tukishampata huyo mtu, mpe timu Julio na Minziro, stars itacheza World Cup"
Binafsi mimi naungana na shaffih kukubaliqna na kauli hii, Mkurugenzi wa ufundi ndiye anayechora mfumo wa mpira wa nchi, mfumo ambao ni kama ramani ya nyumba, kwamba mwenye nyumba anakuwa na ramani then fundi akija anamwambia nataka unijengee nyumba ya ramani hii.
Ukienda nchi kama Nigeria unajua aina ya mpira wao, nchi ya Cameroon tunafahamu aina ya mpira wao, Spain hakuna asiyejua aina ya mpira wao, German mpira wao unajulikana, England wote tunafahamu wanachezaje. Haya yote ni kazi ya mkurugenzi wa ufundi kutengeneza mfumo wa nchi ambao utawekwa mpaka kwenye vilabu vinavyoehiriki Ligi ya nchi. Angalia leo, ikicheza Barca huoni tofauti na timu yao ya taifa. Ikicheza Bayern pia huoni tofauti na timu yao ya taifa ya German.
Lakini Tanzania kila mtu na mfumo wake Toto anacheza hivi, Manyema vile, Yanga nao na mfumo wao, hatuwezi kufika. Husikii watu wakisema!! Ukitaka soka la burudani fuatilia ligi ya Spain, ukitaka mpira nguvu nenda Bunda sliga, hapo hukuti timu moja au mbili zinacheza hivyo, la ni timu zote zina mchezo mmoja.
Kwa hiyo naiomba TFF itafute Expert wa masuala ya ufundi katika soka toka nchi zilizoendelea hasa England au Italy kutokana na aina ya wachezaji wetu. Huyu atasaidia kutengeneza mfumo wa pamoja na kusimamia soka letu kwa ujumla.
Nipo tayari hata kupendekeza majina ya Experts hao
 
Hilo wazo TFF hawana wao na vilabu vyao wanafikiri kushinda ni lazima uwe na kocha mzuri tu basi.
Kiukweli wazo zuri na ndiyo wenzetu waendelea wanatumia mifumo kama hiyo. Kocha mzawa ila wanaajili mkurugenzi wa ufundi ambaye ni mtaalamu.
 
Naunga mkono hoja, hili likifanyika kikamilifu naamini tutapiga hatua.
 
Kwa nchi hii ilivyo nadhani itakuwa ngumu kama vazi la taifa.
 
Tatizo la mpira wa Tanzania ni dogo sana
ila hakuna anaetaka kulitazama

hatujawahi kuwa na programme ya under 17 na under 20 ya kueleweka
ni hapo tu..tukiweza hapo tunacheza popote
 
at the same time most of Tanzanians players believe in superstitious, kupigana misumari., shafii aliona mbali coz yupo exposure.
 
Tatizo la mpira wa Tanzania ni dogo sana
ila hakuna anaetaka kulitazama

hatujawahi kuwa na programme ya under 17 na under 20 ya kueleweka
ni hapo tu..tukiweza hapo tunacheza popote

Hizo zote zipo ndani ya mfumo ambao utachorwa na huyu mkurugenzi. Hao under 17 na under 20 watacheza kwenye mgumo upi wa mpira? Lazima tuwe na mtazamo mmoja na mfumo mmoja wa kimpira
 
Ni wazo zuri sana hasa katika kuendeleza mpira wetu,hakuna haja ya kuajiri makocha wakigeni kwa gharama kubwaa huku akiwa chini ya mkurugenzi wa ufundi mzawa anayezidiwa weledi na kocha mkuu wa timu ya taifa ambaye ni mgeni.Tutafute mkurugenzi wa ufundi mwenye weledi apewe muda kama miaka mitano atengeneze mfumo ambao nchi itautumia.
 
This is bogus....hamna technical dirwctor wenye ujuzi wa hli ya juu atakuja kufanya kazi tanzania bwana....mzungu yoyote mwenye uelewa wa mchezo na anayejua kai yake vizuri hawezi kuja africa apate tabu. Wote wanaokuja huku wamejichokea.

Suluhisho sahii ni sisi kupeleka watu wakasome huko waje hapa nchini wafanye mambo na longo longo ziishe but unfortunately education ndio downfall ya soka la bongo
 
Egland wana mfumo lakini wanaangukia pua kila mara
 
This is bogus....hamna technical dirwctor wenye ujuzi wa hli ya juu atakuja kufanya kazi tanzania bwana....mzungu yoyote mwenye uelewa wa mchezo na anayejua kai yake vizuri hawezi kuja africa apate tabu. Wote wanaokuja huku wamejichokea.

Suluhisho sahii ni sisi kupeleka watu wakasome huko waje hapa nchini wafanye mambo na longo longo ziishe but unfortunately education ndio downfall ya soka la bongo

Hii ndiyo shida ya madaktari wa mifugo kuwa wachambuzi wa soka.
Toto Africa ambayo imedroo jana na simba ina makocha watatu wa kiwango cha kutambulika na shirikisho la mpira barani ulaya (UEFA), lakini wanajitolea tu kufanya kazi pale toto. Unajua kwa nini?
Wanatengeneza CV zao na kujenga uzoefu.
Tangaza kazi ya technical Director wa TFF uone watakaotuma maombi yao mpaka hutoamini kwamba hata huyu naye kaomba!!!!
 
hii ndiyo shida ya madaktari wa mifugo kuwa wachambuzi wa soka.
Toto africa ambayo imedroo jana na simba ina makocha watatu wa kiwango cha kutambulika na shirikisho la mpira barani ulaya (uefa), lakini wanajitolea tu kufanya kazi pale toto. Unajua kwa nini?
Wanatengeneza cv zao na kujenga uzoefu.
Tangaza kazi ya technical director wa tff uone watakaotuma maombi yao mpaka hutoamini kwamba hata huyu naye kaomba!!!!

kutanganza obviously utapata but that dont mean they the best, the best love to work with the best. Simple. Kama alivyosema mourinho africa is for coaches that dont bliv in their abilities.

SECOND KAMA UMESOMA VIZURI KATIKA HIYO UEFA LICENSES WAO WENYEWE WANAKWAMBIA KUWA ATTAINING A UEFA LICENCE DOES NOT GUARANTEE U WILL BE A GOOD/ GREAT COACH, ALL IT DOES IS SATISFY US THAT U KNOW THE FUNDAMENTALS. NI KAMA VILE KUNA WATU WENGI NI MADAKTARI BUT KUNA MADAKTARI BINGWA.
 
Back
Top Bottom