MFIZIGO
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 374
- 233
Maneno haya (sijui kama yeye mwenyewe anakumbuka) aliyazungumza Shaffih Dauda January 2010 baada ya stars kushindwa kufuzu AFCON 2010 na World Cup mwaka huo chini ya maximo.
Katika uchambuzi wake ambao mimi nilimuunga mkono 100% kuwa "tatizo siyo kocha kwa taifa stars, tatizo ni MKURUGENZI WA UFUNDI (Expert). Badala ya kutafuta kocha TFF lazima itafute mtu ambaye ni expert kutoka katika nchi zilizo endelea kama vile Argentina au Spain kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa mpira wetu nchi. Tukishampata huyo mtu, mpe timu Julio na Minziro, stars itacheza World Cup"
Binafsi mimi naungana na shaffih kukubaliqna na kauli hii, Mkurugenzi wa ufundi ndiye anayechora mfumo wa mpira wa nchi, mfumo ambao ni kama ramani ya nyumba, kwamba mwenye nyumba anakuwa na ramani then fundi akija anamwambia nataka unijengee nyumba ya ramani hii.
Ukienda nchi kama Nigeria unajua aina ya mpira wao, nchi ya Cameroon tunafahamu aina ya mpira wao, Spain hakuna asiyejua aina ya mpira wao, German mpira wao unajulikana, England wote tunafahamu wanachezaje. Haya yote ni kazi ya mkurugenzi wa ufundi kutengeneza mfumo wa nchi ambao utawekwa mpaka kwenye vilabu vinavyoehiriki Ligi ya nchi. Angalia leo, ikicheza Barca huoni tofauti na timu yao ya taifa. Ikicheza Bayern pia huoni tofauti na timu yao ya taifa ya German.
Lakini Tanzania kila mtu na mfumo wake Toto anacheza hivi, Manyema vile, Yanga nao na mfumo wao, hatuwezi kufika. Husikii watu wakisema!! Ukitaka soka la burudani fuatilia ligi ya Spain, ukitaka mpira nguvu nenda Bunda sliga, hapo hukuti timu moja au mbili zinacheza hivyo, la ni timu zote zina mchezo mmoja.
Kwa hiyo naiomba TFF itafute Expert wa masuala ya ufundi katika soka toka nchi zilizoendelea hasa England au Italy kutokana na aina ya wachezaji wetu. Huyu atasaidia kutengeneza mfumo wa pamoja na kusimamia soka letu kwa ujumla.
Nipo tayari hata kupendekeza majina ya Experts hao