shushushu_mchokozi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2016
- 405
- 265
AhahahahaaaaaUkiwa na dstv utajiepusha na haya[emoji116] [emoji116] View attachment 412731
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AhahahahaaaaaUkiwa na dstv utajiepusha na haya[emoji116] [emoji116] View attachment 412731
TODAYUmemsahau na Mjumbe mwingine muhimu sana MWIGULU NCHEMBA ( YANGA ) Kiongozi wa Hakikisha Yanga inashinda kwa gharama yoyote ile nchini.
kuna tatzo kwanHII NDIO KAMATI YA MASAA 72 ILIYOBATILISHA KADI NYEKUNDU YA JONAS MKUDE NA KUMFUMGIA MARTIN SANYA MIAKA. 2
WAJUMBE
1. MSAFIRI MGOYI (SIMBA) kamati utendaji tff
2.SALUM CHAMA (SIMBA)M/kit chama cha marefa
3.STEVIN MGUTO (SIMBA)mjumbe bodi ya ligi
4. SAID MOHAMED (SIMBA)makam mwenyeki bodi ya ligi
5.BARUHANI MUHUZA (SIMBA)mjube
6.BONIFAS WAMBURA (SIMBA) C.E O. bodi ya ligi
7.JONAS KIWIA (SIMBA)Mkurugenzi wa mashindano tff
8.JOEL BALISIDYA (SIMBA)Afsa wa ligi bodi ya ligi
9.FATMA ABDALLAH (SIMBA) ofice maneger bodi ya ligi
10. CHARLES NDAAGALA (YANGA) katibu chama cha marefa
11.PHELEMON NTAHILAJA (YANGA) mjube
12.ROSE MSAMILA (YANGA) Asst afsa wa ligi bod ya ligi
13.MACHAEL NGOGO (AIJULIKANI) Asst afsa wa ligi bodi ya ligi
Hawa ndio wajumbe walishiriki kikao cha maamuz yaliyo fanyika jana na kwa uhuwiano huu mlitegemea nn kama sio kutoa maamuzi ya ajabu ya kufuta kadi ya mkude na mengine ya siyo faa ili kuwaaminisha wana simba kwamba kweli walionewa katka mchezo uliomalizika kwa sare ya moja mojaView attachment 412872
haters tu haosioni wapi kakosea
We huoni shida hapo? kwa mtindo huu tutang'oa viti vya viwanja vyote Tanzania!kuna tatzo kwan
hahhh nilishangaa sana kwann mashabiki wa burnley hakutoa viti nikakumbuka dunia ya mungu vitu vya mzungu sisi ndio wa africa bwanaaWe huoni shida hapo? kwa mtindo huu tutang'oa viti vya viwanja vyote Tanzania!
Umeandika mengi lakini pengine wewe pekee ndiye huwezi kuona na kujua malalamiko ya kweli dhidi ya waamuzi na yale ya visingizio kama anayotoaga Mourinho!Kutamba ni sehemu ya mpira na inanogesha utamu wa mpira kama waamuzi watakuwa fair hakuna mtu atalalamika.Simba bila kadi nyekundu kila wanapokutana na Yanga hata wakifungwa hawawezi kulalamikia waamuzi na imeshatokea.Tatizo ninyi wachambuzi wa siasa za mpira pia mnamatatizo sana kwa kudhani mnajua kila kitu mnaishia kutoa mapendekezo yasiyotekelezekaTuwe wakweli. TFF na Kamati zake ina udhaifu mkubwa katika kusimamia Ligi Kuu hapa nchini. Wenye makengeza nimekuwa nikiwasikia wakilalama kwamba TFF na Kamati zake inaibeba Yanga. Nashangaa. Hakuhitajiki hata miwani ya plastiki kibaini kwamba:
1. Maamuzi ya TFF na kamati zake ni ya kuabudu Timu tatu kubwa za Dar kwa kuziridhia matakwa yao hata kama ni kinyume na Sheria, kanuni na taratibu zinazotawala mpira wa miguu hapa nchini. Pale mmoja wapo anapobebwa, ndiyo wenzake wawili na washabiki wao ndio hulalamika kwamba mwenzao amebebwa.
2. Anayebisha kwamba Azam haibebwi aseme ruhusa ya kuacha Ligi Kuu na kwenda kucheza bonanza nje ya nchi huku akiwalazimishia wenzake viporo ni nini.
3. Anayebisha kwamba Yanga habebwi aseme nini maana ya hukumu ya Ngoma kumpiga kiwiko mchezaji wa Simba kwenye Ligi ya Msimu uliopita kutotolewa mpaka leo, na imeishia wapi.
4. Anayesema kwamba Simba haibebwi atueleze ilikuwaje kanuni ya mchezaji kuchagua mechi ya kuikosa baada ya kuoneshwa kadi nyekundu ikatumika kabla ya kutangazwa na kuinufaisha Simba pekee, baada ya hapo mlango ukafungwa kwa komeo la chuma na ufunguo ukatoswa baharini. Au aeleze utamaduni wa kufuta kadi bila ya mhusika kuilalamikia umeanza lini hadi hii ya Mkude ikawa angalau ya pili.
Najua kuna wanaonishangaa sizungumzii magoli yanayolalamikiwa na Simba dhidi ya Yanga, lakini mwenye akili ya tafakuri hawezi kulihusisha hilo moja kwa moja na TFF na Kamati zake. Maana hata tukijaalia kuwa ni kweli waamuzi waliboronga kwa makusudi, huo kisheria ni ukorofi wao na si wa TFF na Kamati zake. Lakini anayenufaika na maamuzi yanayoaminika kuwa ni ya kiushikaji siyo Yanga peke yake. Ndio maana hata kwenye mechi hiyohiyo, Yanga nao wanalalamika kwamba mwamuzi aliliweka kwenye mizani pambano hilo mara tu baada ya nyekundu ya Mkude. Julio naye anawalalamikia waamuzi kwa kufungwa na Mbeya City. Na kadhalika. Ni dhambi kupuuza malalamiko ya timu nyengine dhidi ya waamuzi wanapocheza na isiyo Yanga, kwa sababu tu wao ni timu ndogo. Ama tuyape uzito malalamiko ya timu zote dhidi ya marefa uzito sawa na ya Simba dhidi ya Yanga, au yote tuyatupilie mbali.
Nionavyo, majigambo ya kijinga ya viongozi, wachezaji na wapenzi kabla ya michezo yao ndiyo chanzo kikuu cha dhana hii potofu ya timu kubebwa na TFF ilhali hata kama madai ya ubebaji yakithibitika bado hayatoshi kuhitimisha kwamba yamefanywa na TFF na kamati zake. Kusingizia marefa ni mbinu ovu ya wanamajigambo hawa kutawala kushindwa (defeat management) kwao kwenye mechi waliyotangulia kuisema kwamba ' tutashinda kwa hali yoyote, tutawafunga watake wasitake, wapenzi wasiwe na hofu, hakuna timu ya kutufunga, nani kama timu yetu?, wao ni wateja wetu tu, tuna uhakika wa pointi tatu' n.k. Msemaji wa timu hiyo anapoambulia kipigo ama sare huishia kutafuta kisingizio ili asihojiwe kushindwa kwa majigambo yake. Ndio maana makocha wasio tabia hii huwasikii kulalamika hivyo. Kocha wa Burnley hakujigamba kwamba lazima angeifunga Arsenal ndio maana walipofungwa goli linaloweza kuwa kweli la mkono hawakun'goa viti uwanjani.
Ni upuuzi kudhani mechi zetu kuchezeshwa na marefa wa nje ndio kutaondoa ghasia za aina hii viwanjani, kama kudhani kwamba tunahitaji wageni kuongoza Kamati zetu za Uchaguzi ndio malalamiko ya kuibiwa kura yataondoka. Tunachohitaji ni wadau wa timu zetu kujitambua, na kwamba kufungwa siyo lazima maana yake iwe ni ubovu wa timu, na kwamba hakuna timu isiyofungwa, na kwamba waamuzi ni wanadamu na kwa hivyo kukosea kwao ni lazima, na kwamba hakuna namna ya kubadilisha maamuzi ya refa ukiwa ndani au nje ya uwanja, na kwamba mpira haujafikia uadilifu wa kuwa kila anayestahiki ndiye anayefanikiwa kwa mujibu wa anavyostahiki, na kwamba wachezaji nao ni wanadamu na kwa hivyo lazima watakosea mara nyengine hata kusababisha timu kufungwa, na kwamba mpira ni mchezo wa kistaarabu usiohitaji hasira.
Nilidhani hushughuliki tena na VPL, na kwamba hizo habari za Julio umeziona huko kwenye Ligi unayoishughulikia ambayo ndio sijui kama ni EPL au La Liga mkuu!Sijakuelewa vyema kwamba Julio akiacha kufundisha hapa............
Sidhani Kama uko sahihi juu ya upekee wangu katika hili. Walioweka 'like' kwenye maoni yangu hayo wanathibitisha kwamba siko peke yangu. Usichonielewa ni kwamba marefa wana kosea, iwe makusudi au kibinaadam. Lakini hawakosei kwa kuipendelea au kuiuma timu moja tu. Sema mnaolalamikia makosa hayo huwa mnaumwa na timu moja tu. Chengine usichonielewa ni kwamba hata kama waamuzi wanakosea kwa makusudi, hakuna ushahidi kwamba wametumwa na TFF, la sivyo Kamati zake zisingefuta kinyemela kadi ya Mkude au kumfungia refa huyohuyo iliyemtuma. Chenye ushahidi ni kuwa TFF na Kamati zake inazibeba Simba, Yanga na Azam nje ya uwanja kwa kutoa ama kutotoa maamuzi ya kiajabu.Umeandika mengi lakini pengine wewe pekee ndiye huwezi kuona na kujua malalamiko ya kweli dhidi ya waamuzi na yale ya visingizio kama anayotoaga Mourinho!Kutamba ni sehemu ya mpira na inanogesha utamu wa mpira kama waamuzi watakuwa fair hakuna mtu atalalamika.Simba bila kadi nyekundu kila wanapokutana na Yanga hata wakifungwa hawawezi kulalamikia waamuzi na imeshatokea.Tatizo ninyi wachambuzi wa siasa za mpira pia mnamatatizo sana kwa kudhani mnajua kila kitu mnaishia kutoa mapendekezo yasiyotekelezeka
Mkude alimdondosha mwamuzi kwa kumpuga mtama, then mwamuzi aliposimama akamlima red card, baada ya siku tatu kamati ya 'wahuni' inakaa na kuifuta red card na kumpa kalipio mwaluzi, tena bila hata kusoma report ya mechi ile......
HII NDIO KAMATI YA MASAA 72 ILIYOBATILISHA KADI NYEKUNDU YA JONAS MKUDE NA KUMFUMGIA MARTIN SANYA MIAKA. 2
WAJUMBE
1. MSAFIRI MGOYI (SIMBA) kamati utendaji tff
2.SALUM CHAMA (SIMBA)M/kit chama cha marefa
3.STEVIN MGUTO (SIMBA)mjumbe bodi ya ligi
4. SAID MOHAMED (SIMBA)makam mwenyeki bodi ya ligi
5.BARUHANI MUHUZA (SIMBA)mjube
6.BONIFAS WAMBURA (SIMBA) C.E O. bodi ya ligi
7.JONAS KIWIA (SIMBA)Mkurugenzi wa mashindano tff
8.JOEL BALISIDYA (SIMBA)Afsa wa ligi bodi ya ligi
9.FATMA ABDALLAH (SIMBA) ofice maneger bodi ya ligi
10. CHARLES NDAAGALA (YANGA) katibu chama cha marefa
11.PHELEMON NTAHILAJA (YANGA) mjube
12.ROSE MSAMILA (YANGA) Asst afsa wa ligi bod ya ligi
13.MACHAEL NGOGO (AIJULIKANI) Asst afsa wa ligi bodi ya ligi
Hawa ndio wajumbe walishiriki kikao cha maamuz yaliyo fanyika jana na kwa uhuwiano huu mlitegemea nn kama sio kutoa maamuzi ya ajabu ya kufuta kadi ya mkude na mengine ya siyo faa ili kuwaaminisha wana simba kwamba kweli walionewa katka mchezo uliomalizika kwa sare ya moja mojaView attachment 412872