Nilimaikiliza vizuri sana Shafih na nilimuelewa vizuri sana
Tatizo ni Tff na uwanja wa Taifa kukimbilia mapato badala ya uhalisia
Azam wametumia pesa kujenga uwanja wao na kinachopatikana hata kama ni kidogo asilimia kubwa wanapata wao
Lakini kikubwa zaidi ni ADVANTAGE ya kucheza nyumbani ambayo ikitumiwa vizuri italeta point
Malengo ya mashindano ni kupata point zaidi na si pesa zaidi
Kila timu inauwanja wake wa nyumbani ambao Azam wamechagua Chamanzi, kwahiyo kuwalazimisha wachezee Taifa ikicheza na Simba na Yanga tu si sahihi
Mbona akija Mgambo inacheza Chamanzi? Na je mgambo hawahstahili "usalama" kama baadhi wanavyodai?
Swala la mapato uwanja wa nyumbani ni la timu mwenyeji sasa kama baadhi wa kikosa nafasi kwani lazima wote tuingie uwanjani?
Azam anahitaji point kwanza mengine baadae na si pesa kwanza mengine baadae
Kimantiki maana yake ni kwamba mechi za simba na yanga Azam anacheza ugenini mechi zote nne
Qpr uwanja wao ni25elf na Arsenal 80elf lakini hata siku moja mechi ya qpr haiwezi kuchezwa Amirate
Huko mikoani kuna viwanja vibovu Chamanzi nafuu lakini simba na yanga vinacheza ila hapa dar.......
Watu wasichojua kucheza taifa kuna mkwanja mrefu unabaki kulipia uwanja, bado mgao wa ttf bado mgao baraza la michezo nk