Shahada si lazima tena kwa mgombea urais

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,660
Reaction score
6,282
Nanukuu; 88.-(1)
(e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, @au Awe na ujuzi na @uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa itakayomwezesha @kumudu madaraka ya Rais.
 
Last edited by a moderator:
Nanukuu; 88.-(1)
(e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, @au Awe na ujuzi na @uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa itakayomwezesha @kumudu madaraka ya Rais.

Pakaywatek, Inaonekana unaelewa lakini unataka kuleta mbwembwe kwenye maandishi ili mradi tu! Kuharibu. Sasa chukua wasaa soma vizuri sifa hizo anazotakiwa kuwanzao Rais wa nchi. Darasa hili ni la bure kwako na wasomaji wa JF.

"
Sifa za Rais 88.-(1) Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: (a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii na sheria iliyotungwa na Bunge; (b) ni mwenye akili timamu; (c) wazazi wake wote wawili ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano; (d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini; e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, au awe na ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa utakaomwezesha kumudu madaraka ya Rais; (f) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa au mgombea huru" Hizo ndiyo sifa anazopaswa kuwa nazo Rais.

Nakupongeza kwa kuwa mwanajamvi unayeelewa, sasa ongeza bidii na juhudi zaidi kusoma na kuilelewa Katiba Inayopendekezwa.
 
Kwa kweli msiosoma katiba na kusikiliza ya mtaani mna shida. Leo kijana mmoja kanijia na kusema katiba inayopendekezwa sitaipigia kura kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi. Nikamwambia Mahakama ya Kadhi Haimo kwenye Katiba Inayopendekezwa. Akasema mbona viongozi wetu wa Dini wametwambia hivyo. Nikampa nakala asome. Akabaki kimya. Watu wa jinsi hiyo mko wengi ni wavivu wa kusoma ni wepesi wa kusikia na kufuata ulaghai. Nyie!!!
 
Nanukuu; 88.-(1)
(e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, @au Awe na ujuzi na @uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa itakayomwezesha @kumudu madaraka ya Rais.


Sasa kuna tofauti gani ya anachokisema aliyeanzisha mada na wewe. Yeye amelenga kwenye elimu ya mgombea Urais, wewe umejaza vifungu vyote na ambavyo havihusiani na elimu. Kwa mantiki hii wewe na yeye nani mwelewa zaidi?!

Samahani, naona kama ni mgeni humu JF, na unaonekana kama ni mzuri sana kwenye Facebook/ WhatsApp au GlobalPublishers!!
 

Msingi wa hoja ni sifa za Rais. Kwa hiyo maelezo yamelenga kuwaelimisha ambao wanasoma kupitia JF ili kutoa uelewa mpana wa Katiba Inayopendekezwa. Lengo la JF ni kuelimisha zaidi wengi zaidi ya mawazo yako, hivyo usiwe na kinyongo wengine wanapopata elimu muhimu kwa mustakabali wa taifa lao. Usiwe mchoyo wa elimu, uwe taa palipo na giza. Tatizo lako wewe ni mbinafsi acha uchoyo huu sio mtihani.
 

We Mwanamayu uwage muelewa bhana, usichokielewa hapo kitu gani alichokisema Bi. Mwasi? au madarasa yalikupita kipindi kile ukisingizia umande? ameweka hivo vifungu ili uvisome na kuvielewa au la uipitie hiyo Katiba inayopendekezwa wewe mwenyewe kwa kujiridhisha katika hizo sehemu alizokutajia.
 

Sawa. Wasalimie Sikonge!!
 

Naomba muulize, jee shule alienda kusomea ujinga? maana MWASI MWAKENDA kaweka wazi tena ka bold "Darasa hili ni la bure kwako na wasomaji wa JF." sasa huyu Mwanamayu sijui hajamuelewa au ndiyo hivyo tena.

Inapaswa tushukuru Mungu kuwa na watu wa kujitolea kuelimisha jamii kama alivyofanya Mwasi, hata mimi nimefaidika na hicho kifungu.

Ahsante MWASI MWAKENDA, hawa sampuli za akina Mwanamayu wasikukatishe tamaa, endelea kutupa darsa kila uwezapo. Tunahitaji watu kama wewe kwa sana tu.
 
Last edited by a moderator:
e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, au awe na ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa utakaomwezesha kumudu madaraka ya Rais;

Oh, kwa hiyo ni kweli si lazima awe na shahada ya chuo kikuu.

Ila sasa, huo ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa ni kama upi, kwa mfano?

Na unapimwaje?
 
Oh, kwa hiyo ni kweli si lazima awe na shahada ya chuo kikuu.

Ila sasa, huo ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa ni kama upi, kwa mfano?

Na unapimwaje?



Ha ha ha huyu ndio JF Platinum Member hajui uongozi katika ngazi ya taifa ni upi?unatupotezea muda hilo swali ukamuulize Mbunge wako au wewe sio Mtanzania????
 
Kwa nini wewe usilijibu hadi unambie nikamwulize mbunge wangu?


Nimekuambia ukamuulize mbunge wako kwa sababu naona unatupotezea muda, katiba pendekezwa imeweka wazi kiongozi wa umma/katika taifa ni mtu mwenye dhamana katika umma na anayetekeleza wajibu wake na kutumia madaraka yake kwa:- i. Kuzingatia masharti ya Katiba; ii. Kuheshimu wananchi; iii. Kukuza hadhi ya taifa na kulinda heshima ya ofisi anayoitumikia; na iv. Kukuza heshima ya ofisi kwa wananchi


Na tena imeeleza wazi kabis kuwa Kiongozi wa umma atapaswa kuzingatia yafuatayo:- i.Kufanya uteuzi bila ubaguzi
kwa kuzingatia uwezo, sifa na mwenendo unaofaa, ii. Kutoa uamuzi bila kujali udugu,
ukabila, udini, rushwa, na ubaguzi wa aina yoyote. iii. Kutoa huduma pasipo upendeleo
na kwa kufuata maslahi ya umma.

Haya soma mwenyewe kisha utampima kiongozi wako kwa vigezo na mambo yaliyoanishwa hapo ili umchague! kama hujaelewa uliza tu nikupe shule ukawaambie na wenzako!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…