pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,660
- 6,282
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pakaywatek, Inaonekana unaelewa lakini unataka kuleta mbwembwe kwenye maandishi ili mradi tu! Kuharibu. Sasa chukua wasaa soma vizuri sifa hizo anazotakiwa kuwanzao Rais wa nchi. Darasa hili ni la bure kwako na wasomaji wa JF.
"Sifa za Rais 88.-(1) Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: (a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii na sheria iliyotungwa na Bunge; (b) ni mwenye akili timamu; (c) wazazi wake wote wawili ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano; (d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini; e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, au awe na ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa utakaomwezesha kumudu madaraka ya Rais; (f) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa au mgombea huru" Hizo ndiyo sifa anazopaswa kuwa nazo Rais.
Nakupongeza kwa kuwa mwanajamvi unayeelewa, sasa ongeza bidii na juhudi zaidi kusoma na kuilelewa Katiba Inayopendekezwa.
Sasa kuna tofauti gani ya anachokisema aliyeanzisha mada na wewe. Yeye amelenga kwenye elimu ya mgombea Urais, wewe umejaza vifungu vyote na ambavyo havihusiani na elimu. Kwa mantiki hii wewe na yeye nani mwelewa zaidi?!
Samahani, naona kama ni mgeni humu JF, na unaonekana kama ni mzuri sana kwenye Facebook/ WhatsApp au GlobalPublishers!!
Sasa kuna tofauti gani ya anachokisema aliyeanzisha mada na wewe. Yeye amelenga kwenye elimu ya mgombea Urais, wewe umejaza vifungu vyote na ambavyo havihusiani na elimu. Kwa mantiki hii wewe na yeye nani mwelewa zaidi?!
Samahani, naona kama ni mgeni humu JF, na unaonekana kama ni mzuri sana kwenye Facebook/ WhatsApp au GlobalPublishers!!
Msingi wa hoja ni sifa za Rais. Kwa hiyo maelezo yamelenga kuwaelimisha ambao wanasoma kupitia JF ili kutoa uelewa mpana wa Katiba Inayopendekezwa. Lengo la JF ni kuelimisha zaidi wengi zaidi ya mawazo yako, hivyo usiwe na kinyongo wengine wanapopata elimu muhimu kwa mustakabali wa taifa lao. Usiwe mchoyo wa elimu, uwe taa palipo na giza. Tatizo lako wewe ni mbinafsi acha uchoyo huu sio mtihani.
We Mwanamayu uwage muelewa bhana, usichokielewa hapo kitu gani alichokisema Bi. Mwasi? au madarasa yalikupita kipindi kile ukisingizia umande? ameweka hivo vifungu ili uvisome na kuvielewa au la uipitie hiyo Katiba inayopendekezwa wewe mwenyewe kwa kujiridhisha katika hizo sehemu alizokutajia.
e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria, au awe na ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa utakaomwezesha kumudu madaraka ya Rais;
Oh, kwa hiyo ni kweli si lazima awe na shahada ya chuo kikuu.
Ila sasa, huo ujuzi na uzoefu wa uongozi katika ngazi ya taifa ni kama upi, kwa mfano?
Na unapimwaje?
Ha ha ha huyu ndio JF Platinum Member hajui uongozi wa taifa ni nini?naomba hilo swali ukamuulize Mbunge wako au wewe sio Mtanzania????
Kwa nini wewe usilijibu hadi unambie nikamwulize mbunge wangu?