Shahidi awatambua Sabaya na wenzake ndio waliwavamia dukani

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
666
Reaction score
1,277
Shahidi wa pili katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, Numan Jasin (17) amewatambua kwa kuwashika mabegani Sabaya na wenzake.

Shahidi huyo ametoa ushahidi huo leo Alhamisi Julai 22, 2021 Mbele ya Hakimu Mkazi, Odira Amworo amesema Sabaya ndiye alikuwa anatoa amri zote, huku mshitakiwa wa pili alimpa simu kutaka apige nyumbani kufungua milango na wa tatu walikaa naye kwenye gari.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka shahidi huyo amesema awali wakiwa dukani hakuweza kuwatambua kwani kulikuwa na vurugu dukani.

Shahidi huyo amesema watuhumiwa hao waliwaweka chini ya ulinzi kwa takriban saa tatu kuanzia saa 11 jioni, walipigwa, kusachiwa na kuhojiwa na watuhumiwa hao.

Amesema katika duka hilo walikuwa chini ya ulinzi watu nane, ambao ni yeye, mjomba wake Hajirin Saad, Ally ,Mzee Salimu, Annas, Abuu Mansoor, Bakari Msangi na msichana mmoja.

Jasin amesema baada ya kuwa chini na ulinzi baadaye, waliachiwa wenzao na alibaki yeye na mjomba wake ambao walitakiwa kupanda katika gari lililokuwa nje ya duka.

Hata hivyo amesema mjomba wake ambaye alikuwa amefunga aliomba kununuliwa ndizi ili afungue ndipo Sabaya aliwanunulia ndizi moja moja.

Amesema baada ya kuondoka dukani magari yaliwapeleka nyumbani ambapo wakakuta milango imefungwa ndipo alipewa simu kumpigia mama yake na aliongea na kiarabu kumtaka asifungue.

Amesema baadaye walipelekwa kituo cha polisi Arusha na waliandika maelekezo na kupewa dhamana hadi Februari 10 saa 10 jioni.

Amesema kwa kuwa walimaliza mahojiano usiku polisi aliyekuwa anawahoji aliwapa msaada wa gari lake kuwarudisha nyumbani.
Shahidi huyo wa pili anaendelea kutoa ushahidi wake.

Miongoni mwa Maswali mimi sio mwanasheria Ok kama aliweza kuongea na mama yake kiarabu asifungue mlango kwanini hakumwambia aite polisi?

Anyway ngoja tuone wanavyoendelea kumsafisha Sabaya na tuhuma WALIOKUWA wanampaka miaka yote.

KWA KUWA ALIKUWA MTENDAJI
 
Kwa akili yako, unaona kabisa Sabaya yupo na polisi, yeye ni MKuu wa wilaya, polisi wa wilaya wote wapo chini yake, na unategemea amwambie mama yake aite polisi?

wakati ujio wake tu ulikuwa wa kipolisipolisi-yeye ni mtu mwenye mamlaka, na unategemea amwambie mamake amwite mtu mwingine wa mamlaka aliyeop chini yake? na zaidi ya yote, kutokumwambia mamake aite polisi kuja kumwokoa mikononi mwa mkuu wa wilaya, unafikiri ina negate hoja kwamba aliwavamia na kuwafanyia kilichofanyika?

inapunguza uzito wa hoja kwamba yeye alikuwa anatisha sana kiasi kwamba mtu wa kawaida asingefikiria kutoa taarifa polisi?

Amekwisha huyu sabaya, na hata asipokwisha, ile kuvuliwa ukuu wa wilaya na Rais, kuwekwa lockup kwenye choo ya wazi anatita wakati wenzake wote wananusa nnya yake inatosha kuonyesha kiburi chake kimeshushwa hadi kuzimu kama kile cha mfalme Nebukadreza. bado bashite. shubatini kabisa.
 
Kwa hiyo huyo shahidi anasema walikamatwa wakaporwa halafu wakapelekwa Polisi??? Tena walichoporwa ni simu Tecno na laki 3 ??? Hapa hamna kesi, kabla ya Sept mwisho Sabaya atakuwa huru.
 
Siku zote majungu na fitina kamwe hayawezi kushinda, kwa uwezo wa Mungu atamsaidia atashida mtihani huu alio upata.
Dunia ina watu wabaya sana kuliko hata wanyama!

yaani ni bora Mungu ametuwekea kifo, maaana ingekuwa hatufi nadhani tungetaabishana sana.

lkn leo utamtaabisha binaadamu mwezio lkn iko siku utafukiwa chini ya ardhi.

Binaadamu tusitendeane mabaya, tuishi kwa upendo.
 
Shahidi wa pili katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, Numan Jasin (17) amewatambua kwa kuwashika mabegani Sabaya na wenzake.

Shahidi huyo ametoa ushahidi huo leo Alhamisi Julai 22, 2021 Mbele ya Hakimu Mkazi, Odira Amworo amesema Sabaya ndiye alikuwa anatoa amri zote, huku mshitakiwa wa pili alimpa simu kutaka apige nyumbani kufungua milango na wa tatu walikaa naye kwenye gari.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka shahidi huyo amesema awali wakiwa dukani hakuweza kuwatambua kwani kulikuwa na vurugu dukani.

Shahidi huyo amesema watuhumiwa hao waliwaweka chini ya ulinzi kwa takriban saa tatu kuanzia saa 11 jioni, walipigwa, kusachiwa na kuhojiwa na watuhumiwa hao.

Amesema katika duka hilo walikuwa chini ya ulinzi watu nane, ambao ni yeye, mjomba wake Hajirin Saad, Ally ,Mzee Salimu, Annas, Abuu Mansoor, Bakari Msangi na msichana mmoja.

Jasin amesema baada ya kuwa chini na ulinzi baadaye, waliachiwa wenzao na alibaki yeye na mjomba wake ambao walitakiwa kupanda katika gari lililokuwa nje ya duka.

Hata hivyo amesema mjomba wake ambaye alikuwa amefunga aliomba kununuliwa ndizi ili afungue ndipo Sabaya aliwanunulia ndizi moja moja.

Amesema baada ya kuondoka dukani magari yaliwapeleka nyumbani ambapo wakakuta milango imefungwa ndipo alipewa simu kumpigia mama yake na aliongea na kiarabu kumtaka asifungue.

Amesema baadaye walipelekwa kituo cha polisi Arusha na waliandika maelekezo na kupewa dhamana hadi Februari 10 saa 10 jioni.

Amesema kwa kuwa walimaliza mahojiano usiku polisi aliyekuwa anawahoji aliwapa msaada wa gari lake kuwarudisha nyumbani.
Shahidi huyo wa pili anaendelea kutoa ushahidi wake.

Miongoni mwa Maswali mimi sio mwanasheria Ok kama aliweza kuongea na mama yake kiarabu asifungue mlango kwanini hakumwambia aite polisi?

Anyway ngoja tuone wanavyoendelea kumsafisha Sabaya na tuhuma WALIOKUWA wanampaka miaka yote.

KWA KUWA ALIKUWA MTENDAJI
Kwa hiyo hapo hakukuwa na wizi wala unyang'anyi au sio?

Watu hadi wananunuliwa ndizi na kula.
 
Polisi aliyewahoji akawapa lift watuhumiwa kuwarudisha nyumbani.

Ole sabaya aliwapa ndizi mbivu moja moja wafuturu.

Duh......DC kauzu kweli!
kama aliwapa ndizi ili wafuturu basi inaonekana alikuwa mtu mwema kabisa hadi akakumbuka na kujali imani zao, ingekuwa jambazi kweli wala asinge hangaika na mambo hayo.
 
Kwa hiyo huyo shahidi anasema walikamatwa wakaporwa halafu wakapelekwa Polisi??? Tena walichoporwa ni simu Tecno na laki 3 ??? Hapa hamna kesi, kabla ya Sept mwisho Sabaya atakuwa huru.

..tatizo ni mashahidi kudai walipelekwa POLISI.

..Je, Polisi wana rekodi ya Sabaya kuwapeleka watu hao kituoni?

..zaidi, ilikuwaje Sabaya akatoka kituo chake cha kazi wilaya ya HAI, na kwenda Arusha mjini na kufanya hayo anayotuhumiwa nayo?

..tatizo siyo tecno au laki 3, tatizo ni matumizi ya SILAHA ktk tukio analotuhumiwa Sabaya.

..ukiiba simu ya tecno na laki 3 bila kutumia silaha unahesabika kuwa ni mwizi / kibaki / mdokozi.

..ukiiba simu ya tecno na laki 3 kwa kutumia au kutishia kwa SILAHA utashtakiwa kwa UNYAN'GANYI / UJAMBAZI.

..Sabaya itabidi approve mahakamani kwamba alikuwa mahali pengine siku na saa ambayo tukio lilitokea. Kinyume na hayo nadhani kesi hii ni mbaya kwake.
 
kama aliwapa ndizi ili wafuturu basi inaonekana alikuwa mtu mwema kabisa hadi akakumbuka na kujali imani zao, ingekuwa jambazi kweli wala asinge hangaika na mambo hayo.

..tatizo Sabaya alikuwa amewakamata kama nani?

..Sabaya anaweza vipi kutoka mkoa mmoja na kwenda kukamata muuza duka ktk mkoa mwingine?
 
Kwa sisi wenye kufanya kazi ya kutoa haki, ukiona Shahidi amekutambua kwamba wewe ndio uliyefanya tukio unalotuhumiwa, aisee anza kukaa mguu sawa.

Siongezi maneno wengine endeleeni kuongea mnayotaka kuongea.
Wewe sio Mwanasheria muongo Idadi ya watu ilikuwa ndogo ni vipi usiwatambue watu wakiwa dukani alafu badaye uwatambue kama sio ushahidi wakufundishwa ni nini?
 
shahidi anatakiwa aseme alikutambua vipi, alikuwa anakujua kabla (hap sabaya alikuwa anajulikana hata na mimi ninayekaa mkoa wa mbali kabisa), mwanga, (kulikuwa na umeme), umbali (alikuwa karibu kabisa alinichapa hadi kofi na tulitazamana kwa robo saa wakati wa matezo), time spent (karibia nusi, manake taangu afike, atukamate, aanza kutuhoji uso kwa uso, atuchape n.k hadi atupandike kwenye gari), horrific environment (hapakuwa na horro yeyote kwasababu hapakuwepo na urushaji risasi kwamba tungekuwa kwenye hekaheka, ni alifika akatukamata bial kurusha risasi akaanza kutuhoji .nk)...., shahidi akinyoosha haya, sabaya hapangui.
 
Wewe sio Mwanasheria muongo Idadi ya watu ilikuwa ndogo ni vipi usiwatambue watu wakiwa dukani alafu badaye uwatambue kama sio ushahidi wakufundishwa ni nini?

..hili tukio lilisharipotiwa tangu wakati wa Magufuli.

..tatizo serikali ya Magufuli ilikuwa haina utashi wa kumchukulia hatua Sabaya.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
..tatizo Sabaya alikuwa amewakamata kama nani?

..Sabaya anaweza vipi kutoka mkoa mmoja na kwenda kukamata muuza duka ktk mkoa mwingine?
subiri ushahidi. majungu na fitina havina nafasi mbele ya sheria.
mmemchafua sana jamaa wa tu
ukweli na uongo utabainika tu.
 
..does he have an alibi?

..utetezi wa Sabaya utakuwa ni nini?

..Je, utetezi utakuwa kwamba hakutumia silaha?

..Au utetezi utakuwa kwamba hakuwepo kabisa eneo la tukio?

..Je, atakubali kusimama mahakamani na kujitetea, au ataamua kukaa kimya kwa kuogopa kujichanganya / kujichongea?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Wewe sio Mwanasheria muongo Idadi ya watu ilikuwa ndogo ni vipi usiwatambue watu wakiwa dukani alafu badaye uwatambue kama sio ushahidi wakufundishwa ni nini?
Nadhani wewe sio mwanasheria, tusibishane. Au naomba utumie uhuru wako wa kikatiba kuendelea na Imani uliyonayo kwenye hilo unalosimamia.

JF imejaa vijana wajuaji kama meko.
 
Bongo muvi jambazi anamnunulia mtekwaji ndizi ili apate futuru nakisha jambazi anampeleka raia polisi mwenyewe !!!!! Mweeeeeeeee mweeeeee
 
Back
Top Bottom