GE2025 Shahidi wa Jamhuri asema Isingewezekana Mpina kupata Haki kwakua majaji ni wateule wa Rais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Sir John Deere

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
14,246
Reaction score
27,509
Mambo mengine ni kama Mungu kaamua kuwaumbua watesi wa Lissu hadharani.

Leo katika hali ya kushangaza shahidi wa upande wa serikali baada ya kuulizwa je bwana Luhaga Mpina angeweza kupata Haki yake kikatiba ya kugombea urais hasa ukizingatia watoa maamuzi ni majaji walioteuliwa na Rais ? Bwana shahidi alijikuta akiropoka mahakamani kuwa hilo lisingewezakana kamwe.🀣
================
TUNDU Lissu , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeshtakiwa kwa uhaini katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, amekimuuliza maswali ya dodoso shahidi wa pili wa serikali (John Kaaya) alimuuliza kama angewezekana mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo Luhaga Mpina apate haki kwenye mahakama ambayo majaji ni wateule wa rais na ndio mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) shahidi huyo akajibu isingezekana.
 
Na ni maajabu zaidi kuwa ni mahakama haya haya anayotegemewa Tundu Lissu apate HAKI!
Sasa waTanzania tutakimbilia wapi na hali ya namna hii?

Njia pekee iliyo bakia, ni kwa waTanzania "KUKINUKISHA, tena sana"!
 
Tayari Lissu anachofanya huko mahakamani ni kupambania HAKI sisi Wananchi ndio Bado tumelala.
 
Na ni maajabu zaidi kuwa ni mahakama haya haya anayotegemewa Tundu Lissu apate HAKI!
Sasa waTanzania tutakimbilia wapi na hali ya namna hii?

Njia pekee iliyo bakia, ni kwa waTanzania "KUKINUKISHA, tena sana"!
Hiyo ni "Big Ask"kwa watanzania ambao leo hii balozi wa nyumba kumi kapewa baiskeli na fedha kidogo za kujikimu kwa wakti huu hadi uchaguzi.

Lakini huenda ni haohao mabalozi wa nyumba 10 na viongozi wa serikali za mitaa wana maelekezo maalum ya kuhakikisha wazitoa taarifa za kupelekea watu kukamatwa na wasojulikana.

2020 CCM haikuwa na kazi ngumu ingawa nguvu kubwa ilitumika na angalau Lissu akashiriki uchaguzi ambao ulijaa mizengwe. Safari hii Chadema imeondolewa kwenye uchaguzi na kiongozi wake Lissu yuko mahakamani na uwanja wa siasa uko wazi kwa CCM kujitangaza washindi.

Isitoshe, safari hii uchaguzi umegharamiwa na wenye pesa na wamewekeza mabilioni (kupitia ile harambee)na njia zingine ili kuhakikisha CCM yabakia madarakani, hivyo hao wategemea malipo mazuri baada ya ushindi wake.

Labda iwe miujiza lakini jinsi vyombo vilivyoandaliwa na posho na magari na zana zote zikiwemo silaha kali, na kuambiwa kwatakiwa utulivu mkuu, KUKINUKISHA ni "Big Ask".
 
Hii kesi ya uhaini wa mchongo inamuumbua Sir100 na vijibwa vyake vilivyomuingiza mkenge.
 
Labda iwe miujiza lakini jinsi vyombo vilivyoandaliwa na posho na magari na zana zote zikiwemo silaha kali, na kuambiwa kwatakiwa utulivu mkuu, KUKINUKISHA ni "Big Ask".
Haijawahi kutokea; NATAKA NIRUDIE KWA MSISITIZO; HAIJAWAHI KUTOKEA..., wakati mzuri na sahihi kabisa kwa waTanzania kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii kama ilivyo wakati huu.
Itakuwa bahati mbaya sana endapo waTanzania hawataitumia nafasi hii adimu sana kuleta mabadiliko ndani ya nchi yao.

Yote hayo ya hao viongozi wa mitaani na mengineyo; hayo ni mapambo ya hadaa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…