Shahidi wa mwajiri agoma kutokea kwenye hearing

ngofoman

Member
Joined
Jan 8, 2023
Posts
53
Reaction score
39
Habari wakuu wa sheria, nimekuja mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba msaada wa kishelia.
Nitajitahidi kuifupisha kadri iwezekanapo lakini mtaelewa ninachoomba kutoka kwenu.
Mimi nilikuwa ni mtumishi kwenye taasisi moja binafsi, nimefanya kazi kwa miaka zaidi ya ishirini kwenye hio taasisi. Hivi karibuni taasisi hio amekuwa ikifanya vibaya na kushindwa kujiendesha kutokana na kupata ushindani wa kibiashara. Wafanyakazi waliofanya miaka mingi kwenye hio kampuni wameanza kufukuzwa kazi kwa makosa yasio na maana yoyote tena wanafukuzwa bila malipo. Kuna baadhi ya wafanyakazi wamefukuzwa kwa kesi za kutengenezwa. Mimi pia ni mmoja wa wafanyakazi ambao tumefukuzwa kazi kwa kutengenezewa kesi ili nisilipwe haki zangu.

Mambo ya kisheria ninayohitaji kujua ambayo yamenileta hapa.

1. Ni haki mfanyakazi mdogo kufukuzwa kazi kwa makosa yaliofanywa na meneja wake? Nimefukuzwa kazi kwa madai kwamba nilifahamu meneja wangu anamahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi mwenzake lakini mimi sikuripoti. Wanasema kosa langu ni gross negligence ( uzembe mkubwa) Naomba angalieni hapo kama kutokuripoti kumefikia levo ya kuitwa gross negligence.

2. Shahidi wa mwajili ambaye ni yule binti aliyekuwa anatoka kimepenzi na meneja wangu alitakiwa kufika kwenye hearing ili aeleze mimi nilijuaje kama anamahusiano na meneja wangu, kwa sababu yeye ndiye aliyesema mimi nilikuwa najua. Shahidi huyo hakufika kwenye hearing kwa sababu ni mjamzito na hajisikii vizuri. HR aliamua kumpigia simu na kuweka loud speaker ili aweze kutoa ushahidi kupitia simu. Kishelia hii inaruhusiwa, mwajili anampigia simu shahidi wake atoe ushahidi kwa njia hio?

3. Nilipopewa nafasi ya kumwuliza maswali huyo dada nilimwuliza swali moja kwamba kwa nini aliniambia mimi kama anatoka kimapenzi na meneja wangu, huyo dada akaanza kulia kisha akakata simu. HR akaniambia niulize maswali mepesi kwa sababu shahidi wake hajisikii Vizuri. Kisheria hapo nimetendewa haki?

Mwisho wa yote mwajili akanifukuza kazi kwa kosa la kutoripoti. Naomba wajuzi wa sheria waangalie hapo kama kisheria ilitakiwa kufukuzwa kazi au ni njia tu ya kuniibia mafao yangu ya utumishi wa muda mrefu.

Kama kuna ufafanuzi utahitajika niko tayari kuongezea hapo nimeandika kiufupi.

Nawasiliaha wakuu.
 
Ushahidi wa kuweka loudspeaker sijawahi kuusikia na mtu akiwa kwenye mapenzi unajuaje unakua unawachungulia au vipi? Kesi ndogo hiyo kata rufaa
 
Uliajiriwa ufanye kazi yakumchunguza meneja au kazi yako inahusiana na nini haswa ?

Sababu ya uzembe ndo huo wakushindwa kuripoti mahusiano ya meneja wako ?
 
Uliajiriwa ufanye kazi yakumchunguza meneja au kazi yako inahusiana na nini haswa ?

Sababu ya uzembe ndo huo wakushindwa kuripoti mahusiano ya meneja wako ?
Mimi hata haikuwa kazi yangu, mimi nilikuwa supervisor wa ulinzi
 
Mimi hata haikuwa kazi yangu, mimi nilikuwa supervisor wa ulinzi
Sababu ndio hio mkuu sikuripoti na mimi sio mfanyakazi wa kupokea kesi hizo mimi nilikuwa supervisor wa ulinzi sasa meneja wangu ndio inasemekana alikuwa na mahusiano naye, meneja mwenyewe hajawahi kuniambia
 
Ndugu wahi CMA haraka kafungue kesi,hapo unaweza kupiga mpunga mrefu sana kama fidia! Kesi nyepesi mnoo kwako....ila tafuta wakili .....akikusimamia vizuri naiona 500m hapo
 
Ndugu wahi CMA haraka kafungue kesi,hapo unaweza kupiga mpunga mrefu sana kama fidia! Kesi nyepesi mnoo kwako....ila tafuta wakili .....akikusimamia vizuri naiona 500m hapo
Kampuni yenyewe haifikishi hizo pesa mkuu. Itakuwaje?πŸ˜†πŸ˜†
 
Ndugu wahi CMA haraka kafungue kesi,hapo unaweza kupiga mpunga mrefu sana kama fidia! Kesi nyepesi mnoo kwako....ila tafuta wakili .....akikusimamia vizuri naiona 500m hapo
Ahsante mkuu yaani sikupata usingizi siku mbili, sikuwahi kutumia dawa ya usingizi lakini sasa nimetumia. Nilikuwa nafanya kazi kwa bidii sana mpaka nikawa napewa recognition certificates na appreciation certificates, sasa wamebadili viongozi wazuri na kuweka Wakenya ndio wanafukuza sana wafanyakazi.
 
Kampuni yenyewe haifikishi hizo pesa mkuu. Itakuwaje?πŸ˜†πŸ˜†
Ni global company mkuu, mwanzo office zao zilikuwa London, kipindi hicho kampuni ilikuwa ikifanya vizuri na wafanyakazi walikuwa na furaha lakini tangu walipohamishia office Kenya wakenya wengi wamekuwa wakija Tanzania na kufukuza wafanyakazi kwa kesi za ajabu
 
Wakenya wasenge sana ikiwezekana wachome uhamiaji
 
Wapeleke chapu mahakamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…