Habari wakuu wa sheria, nimekuja mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba msaada wa kishelia.
Nitajitahidi kuifupisha kadri iwezekanapo lakini mtaelewa ninachoomba kutoka kwenu.
Mimi nilikuwa ni mtumishi kwenye taasisi moja binafsi, nimefanya kazi kwa miaka zaidi ya ishirini kwenye hio taasisi. Hivi karibuni taasisi hio amekuwa ikifanya vibaya na kushindwa kujiendesha kutokana na kupata ushindani wa kibiashara. Wafanyakazi waliofanya miaka mingi kwenye hio kampuni wameanza kufukuzwa kazi kwa makosa yasio na maana yoyote tena wanafukuzwa bila malipo. Kuna baadhi ya wafanyakazi wamefukuzwa kwa kesi za kutengenezwa. Mimi pia ni mmoja wa wafanyakazi ambao tumefukuzwa kazi kwa kutengenezewa kesi ili nisilipwe haki zangu.
Mambo ya kisheria ninayohitaji kujua ambayo yamenileta hapa.
1. Ni haki mfanyakazi mdogo kufukuzwa kazi kwa makosa yaliofanywa na meneja wake? Nimefukuzwa kazi kwa madai kwamba nilifahamu meneja wangu anamahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi mwenzake lakini mimi sikuripoti. Wanasema kosa langu ni gross negligence ( uzembe mkubwa) Naomba angalieni hapo kama kutokuripoti kumefikia levo ya kuitwa gross negligence.
2. Shahidi wa mwajili ambaye ni yule binti aliyekuwa anatoka kimepenzi na meneja wangu alitakiwa kufika kwenye hearing ili aeleze mimi nilijuaje kama anamahusiano na meneja wangu, kwa sababu yeye ndiye aliyesema mimi nilikuwa najua. Shahidi huyo hakufika kwenye hearing kwa sababu ni mjamzito na hajisikii vizuri. HR aliamua kumpigia simu na kuweka loud speaker ili aweze kutoa ushahidi kupitia simu. Kishelia hii inaruhusiwa, mwajili anampigia simu shahidi wake atoe ushahidi kwa njia hio?
3. Nilipopewa nafasi ya kumwuliza maswali huyo dada nilimwuliza swali moja kwamba kwa nini aliniambia mimi kama anatoka kimapenzi na meneja wangu, huyo dada akaanza kulia kisha akakata simu. HR akaniambia niulize maswali mepesi kwa sababu shahidi wake hajisikii Vizuri. Kisheria hapo nimetendewa haki?
Mwisho wa yote mwajili akanifukuza kazi kwa kosa la kutoripoti. Naomba wajuzi wa sheria waangalie hapo kama kisheria ilitakiwa kufukuzwa kazi au ni njia tu ya kuniibia mafao yangu ya utumishi wa muda mrefu.
Kama kuna ufafanuzi utahitajika niko tayari kuongezea hapo nimeandika kiufupi.
Nawasiliaha wakuu.