Shahidi wangu kagoma kwenda kutoa ushahidi

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Katika kesi inayonikabili baada ya kuendelea hapa mahakama ya mwanzo. Kufikia upande wa shahidi wa utetezi yaani mimi kama mtuhumiwa.
Mbele ya hakimu nlisema ninao mashahidi 2, ambao ni mtu ninaeishi nae na mpaka siku natajwa na mshitaki kuwa aliniona nikimuibia nlikuwa kwangu na ninaeishi nae.

Shahidi wa pili ni jirani wa karibu ambae mshitaki alimuita asubuhi amfungulie mlango baada ya kufungiwa nje usiku.


Shahidi huyu wa pili aligoma kuwa shahidi wa mshitaki kwani alikuwa rafiki wake wa karibu sana lakini walikuja kukwazana na kugombana baada ya mshitaki kutengeneza tukio la kuibiwa na kudai aliniona mimi usiku nikimuibia.

Alihitaji huyo jirani ake awe shahidi wake lakini kutokana na uongo ambao angeenda kuhushahidia jirani ake amegoma na mshitaki aliamua kuhama kabisa na hata kabla ya kesi haijaisha.

Kwa upande wangu nilimtaja huyo jirani ake kama shahidi wangu baada ya kuona mshitaki anaidanganya mahakama kuwa alipiga kelele usiku hakusikika na alifunguliwa mlango usiku ule ule wakati ukweli ni kuwa alifunguliwa mlango asubuhi saa moja na jirani ake huyo.

Nimemuomba jirani ake huyo akantolee ushahidi juu ya mda alomfungulia mlango mshitaki na kutokusikika kwa kelele siku ya kuibiwa lakini amegoma kwa kudai mpaka apatiwe samasi ya kwenda huko.

Je kwa upande wangu naweza kuieleza nini mahakama juu ya kutokufika kwashahidi huyu?
Na ni shahidi muhimu sana kwa upande wangu.

Nawasilisha............
 
Kwani ulimwambia tu kwq maneno?? Witness summon/ subpoena sio ombi, kama alipewa hii hamna jinsi, akikwepa ni kosa na laweza muweka ndani.
 
Muoombee summon mahakaman ili aweze Fika hakikisha anaisaini.ili akikataa akakamatwe..
 
Sasa mkuu wewe unataka umbebe tu bila ya kuwa na court summons, mfano ni mfanya kazi anaaga vipi kazini au anaomba vipi ruhusa atasema anaenda mahakamani kutoa ushahidi huku akiwa hana hata cha kuonyesha kazini kama kweli kaitwa kutoa ushahidi.

Shahidi anapaswa kupewa summons na mahakama akijulishwa yeye ni miongoni mwa mashahidi ktk kesi flani na anatakiwa kuwa mahakamani siku flani kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.

Asipokuja sasa kutoa ushahidi hiyo inakua juu ya mahakama ni hatua gani za kuchukua na hapo lazima warrant of arrest itakua issue na atakamatwa na kuwekwa ndani kwa contempt of tha court (kuidharau mahakama)
 
Asante mkuu kwa ushauri nashukuru sana ntafanya hivyo
 
Hata mimi ukinifuata bila court summons nakataa,kwani kuzuri kule mahakamani mpaka tubebane tu kupelekana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…