Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
ACT WAZALENDO YACHARUKA HUJUMA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KYANG'OMBE, RORYA
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu ametoa Wito kwa Waziri wa TAMISEMI kumuwajibisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa kuruhusu Mradi wa Kituo cha Afya Kata ya Kyang'ombe kujengwa chini ya kiwango.
Ado alitoa kauli hiyo alipokagua ujenzi wa Kituo hicho cha afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi na michango ya wahisani.
"Ndugu Mchengerwa tupia jicho lako hapa Kata ya Kyang'ombe Wilaya ya Rorya. Diwani amenijulisha kuwa wananchi wamechangishana fedha na shirika la NMB limechangia fedha Mil. 15 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya. Nimesikitishwa kuelezwa kuwa Wataalamu wa Halmashauri wameutelekeza mradi huu na Mkandarasi anajenga chini ya kiwango bila mwongozo wa Injinia wa Halmashauri ambaye amekataa kuja kwenye mradi. Nimekuta mbao za kuezekea kituo hicho cha afya zikiwa duni na mkandarasi anafanya anavyotaka mwenyewe. Hii ni dalili ya rushwa na Wizara inapaswa kuchukua hatua"-alisema Ndugu Ado