sanalii
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,639
- 5,767
Paukwa tena pakawa, mtaani taharuki
Bibi kanyoa kipara, na nywele tena hasuki
Chaajabu kina chawa, kichwani hawabanduki
Bibi kanyoa kipara, mtaani taharuki
Mtaani wauliza, hiki kipara chanini
Mana wengi chawaliza, madukani na saluni
Ma tena chaleta giza, biashara taabani
Bibi kanyoa kipara, mtaani taharuki.
Tena kichwa kina chawa, hutuwezi kukigusa
Bibi anaona sawa, ni vigumu kukumbushwa
Akiosha kwenye bwawa, hadi maji yakaushwa
Bibi kanyoa kipara, mtaani taharuki
Babu alikua nacho,ila chake tofauti
Na chawa walikuepo, ila shingo hawavuki
Mafuta akipakako, hata yale ya kinafiki
Bibi kanyoa kipara, mtaani taharuki
Babu alipokiosha, hakutaka maji mengi
Majumbani yalitosha, yakabaki kwenye tenki
Hapo safi babu ngosha, wavuvi mambo hayendi
Bibi kanyoa kipara, mtaani taharuki
Bibi hafiki mtoni, ili anawe vizuri
Hata pale kifukoni, anapaona kwa mbali
Nailiza kulikoni? hiki kipara cha dili