Shairi: Damu ya Albino

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Kwa pamoja tuungane na kuwatetea ndugu zetu hawa wenye ulemavu wa ngozi.
1>damu yake yamwagika,bila hata ya hatia.
Na vilio vya sikika.,maumivu wasikia.
Yamewajaa mashaka,kipi walichokosea ?
Damu ya maalibino,nani ataja ilipa ?
2>damu itatulaani,kosa tukiendeleza.
Wauaji ni motoni,wao waamini giza.
Watajutia rohoni,na aliewapoteza.
Damu ya maalibino,nani ataja ilipa ?
3>damu yao itasema,kwanini tuliuliwa.
Siku ile ya kiyama,hukumu kuhukumiwa.
Hakuna ataesema,motoni kuchuliwa.
Damu ya maalibino,nani ataja ilipa ?
4>damu yao siyo maji,ipotee hivi hivi.
Damu yao si mtaji, ichezewe kama hivi.
Hakika kila muwaji,si mtu nyakati hizi.
Damu ya maalibino,nani ataja ilipa ?
5>maswali tujiuze,hadi jibu tulipate.
Tuache kupiga zeze,makubwa yasitupate.
Na tena tuwakimbize,wauaji tuwapate.
Damu ya maalibino,nani ataja ilipa ?
Shairi:damu ya albino.
Mtunzi:Idd Ninga

Maoni=iddyallyninga@Gmail.com

"DAIMA TUTAWAKUMBUKA MILELE,KAMA WATANZANIA HAWATOWATAZAMA,BASI MUNGU ATAWASHIKA MKONO,MSIOGOPE HAKUNA HAKI ITAKAYOPOTEA,ISIPOLIPWA DUNIA,ITAJALIPWA MBINGUNI"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…