LwandaMagere
JF-Expert Member
- Mar 15, 2020
- 264
- 2,484
Gari...gari...gari...gari..!! Una nini wewe?
Gari hata kama chakavu,heshima hukupatia,
Haijalishi uwe mkubwa hata mdogo pia,
Dunia yote inatambua,matajiri na masikini pia,
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?
Gari huleta heshima,hata kama ilipotea,
Ndugu watakunyenyekea,iwe hiari au lazima,
Gari huleta kibri,na majivuno pia,

Gari huleta heshima,hata kama umepanga,
Haijarishi ni kimara,ubungo hata kule upanga,
Gari haina macho,watu njiani maji kuwamwagia,

Mademu hujigonga,hata kama una sura mbaya,
Gari huwavutia,hata kama hukuwa na nia,
Wengi utawagonga,kina amina hata sara pia,

Waswahili husema,Gari ni uchawi wa mzungu,
Hii kauli hunipa wazimu,macho hujaa ukungu,
Nyumba hazina thamani,thamani ni uchawi wa mzungu,

Jamani ndugu zangu,wanajamvi wenzangu,
Nijenge nyumba yangu,au ninunue gari yangu?
Niwakakaribishe Kwangu Au kwenye gari yangu?

Mwanamke anathamini gari
Ndugu wanathamini gari
Marafiki hukuona wa thamani unapokuwa na gari.
Kwenye vikao hupewa kuchangia unapokuwa na gari.
Gari...Gari....Gari...Gari...Gari...Gari....Gari...Gari...
Nyumba hazina thamani tena kila kitu ni Gari
Nauliza ndugu zangu kati ya Gari na nyumba bora nini?
Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..[emoji382]