SHAIRI: Gari una nini wewe?

SHAIRI: Gari una nini wewe?

LwandaMagere

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2020
Posts
264
Reaction score
2,484
Gari...gari...gari...gari..!! Una nini wewe?

Gari hata kama chakavu,heshima hukupatia,
Haijalishi uwe mkubwa hata mdogo pia,
Dunia yote inatambua,matajiri na masikini pia,
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?

Gari huleta heshima,hata kama ilipotea,
Ndugu watakunyenyekea,iwe hiari au lazima,
Gari huleta kibri,na majivuno pia,
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?

Gari huleta heshima,hata kama umepanga,
Haijarishi ni kimara,ubungo hata kule upanga,
Gari haina macho,watu njiani maji kuwamwagia,
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?

Mademu hujigonga,hata kama una sura mbaya,
Gari huwavutia,hata kama hukuwa na nia,
Wengi utawagonga,kina amina hata sara pia,
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?

Waswahili husema,Gari ni uchawi wa mzungu,
Hii kauli hunipa wazimu,macho hujaa ukungu,
Nyumba hazina thamani,thamani ni uchawi wa mzungu,
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?

Jamani ndugu zangu,wanajamvi wenzangu,
Nijenge nyumba yangu,au ninunue gari yangu?
Niwakakaribishe Kwangu Au kwenye gari yangu?
Afrika bara langu,hivi ni wapi tunakosea?

Mwanamke anathamini gari

Ndugu wanathamini gari

Marafiki hukuona wa thamani unapokuwa na gari.

Kwenye vikao hupewa kuchangia unapokuwa na gari.

Gari...Gari....Gari...Gari...Gari...Gari....Gari...Gari...

Nyumba hazina thamani tena kila kitu ni Gari

Nauliza ndugu zangu kati ya Gari na nyumba bora nini?

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..[emoji382]
 
Hata mie niliponzwa na Nissan Patrol Nyeupe isiyo na tinted, kutoka mataa ya Maktaba maeneo ya Posta mpya hadi mataa ya mbuyuni maeneo ya namanga... tukabaki kupungiana mikono tuu na tabasamu la mbaalii kiasi cha kushikwa na butwaa nisimfuate au yeye anifuate....

Foleni ilinogesha utamu maana kila tukipishana lazima tutizamane na kutabasamu aahahahaa mwisho akapiga honi pyee nami nikamjibu pyiii na kupunga mkono ila karoho kaliniumaaa....

Ndo ilikuwa Crush yangu ya kwanza tangu hapo magari hayajaniacha salama hata kidogo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]pole sana mkuu

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..[emoji382]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hata mie niliponzwa na Nissan Patrol Nyeupe isiyo na tinted, kutoka mataa ya Maktaba maeneo ya Posta mpya hadi mataa ya mbuyuni maeneo ya namanga... tukabaki kupungiana mikono tuu na tabasamu la mbaalii kiasi cha kushikwa na butwaa nisimfuate au yeye anifuate....

Foleni ilinogesha utamu maana kila tukipishana lazima tutizamane na kutabasamu aahahahaa mwisho akapiga honi pyee nami nikamjibu pyiii na kupunga mkono ila karoho kaliniumaaa....

Ndo ilikuwa Crush yangu ya kwanza tangu hapo magari hayajaniacha salama hata kidogo.
ungana na mtu fulani muhimu alipata kusema,

".... usinibabaishe natongozwa na wenye pesa zao, na wenye magari yao"

mpaka leo inaniuma lakini najipa moyo kuna siku nitamtafuta @PRONDO anielekeze wapi kuna vitz nikasuuze machungu.

have a nice Monday Kassie! you raised my painful memories!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah umenikumbusha shauri la Mpwa wangu Mentor INSIDE VEROSSA lilisambaa hadi kwenye mitandao mingine
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ungana na mtu fulani muhimu alipata kusema,

".... usinibabaishe natongozwa na wenye pesa zao, na wenye magari yao"

mpaka leo inaniuma lakini najipa moyo kuna siku nitamtafuta @PRONDO anielekeze wapi kuna vitz nikasuuze machungu.

have a nice Monday Kassie! you raised my painful memories!

Sent using Jamii Forums mobile app

Usiweke mabaya moyoni, unauongezea kazi moyo zaidi ya ile kuu ya kusukuma damu eehehehee.

Huyu uliyemuita ni swahiba wangu wacha nimguse bega akusikilize hitaji lako...

Baba Batalungaya.....

Njooo, inaitwa huku.... RRONDO
 
Back
Top Bottom