SHAIRI: Kipini cha Pini

SHAIRI: Kipini cha Pini

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
Kipini Cha Pua

1
Silifanyi siri tena, ninasema hadharani
Vyuma vinafumuana, nionapo manjiani
Shufu sinayo maana, urembo wenu ficheni
Avaae hupendeza, nami chanipa uchizi

2
Kiwe cha rangi ya silva, kivaliwe na mweusi
Mdomo rangi 'meiva, sare kope pamwe nyusi
Gauni liwe la nguva , kisha asiwe kamasi
Avaae hupendeza, nami chanipa uchizi

3
Vipo pia vya dhahabu, mapambo rangi ya fedha
Kisipotiwa hijabu, kinaweza kupa adha
Nyeupe istihibabu, wapenda sana mabudha
Avaae hupendeza,nami chanipa uchizi

4
Icho kipini cha pua, ndicho chanipa uchizi
Sende huko kuagua, ukaipewa hirizi
Bure tu utanigua, wakivao ni wajuzi
Avaae hupendeza,nami chanipa uchizi

Abuuabdillah [emoji3578][emoji1241]
0744883353
Jumaomari5@gmail.com
 
Kipini Cha Pua

1
Silifanyi siri tena, ninasema hadharani
Vyuma vinafumuana, nionapo manjiani
Shufu sinayo maana, urembo wenu ficheni
Avaae hupendeza, nami chanipa uchizi

2
Abuuabdillah [emoji3578][emoji1241]
0744883353
Jumaomari5@gmail.com

Ugonjwa wake Vipini!!

Ninaazia salamu, kujibu bin fulani
Kaelezea ugumu, avionapo vipini
anaipata na hamu, na kuihisi mwilini
Ugonjwa wake vipini, kwa wanakwake puani!

Kwa ari kaelezea, kwake huo mtihani
Ashindwa kujizuwia, avionapo puani
Ashiki yampandia, avurugikwa kichawni!
Ugonjwa wake vipini, avionaapo puani!

Vyeupe ama vya rangi, alimuradi vipini
Utadhania msingi, kupenda mwana fulani
Aina zake ni nyingi, nivisemavyo vipini
Ugonjwa wake vipini, avionapo puani!

Na roho humripuka, kasema bila utani!
Hapo yeye kahemka, kasema yalo moyoni
Musije mkamcheka, ugonjwa wake mtani
Ugonjwa wake vipini, avionapo puani!

Tano nasema tamati, nawa ageni juweni
Ni mwisho si katikati, namalizia betini
Siyo kama mwala buti, ni mwisho wa kituoni!
Ugonjwa wake vipini, avionapo puani!!


"Choveki"
 
Back
Top Bottom