Shairi Kula ilonona

Shairi Kula ilonona

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
Kula ilonona

Niliyowaza ni mengi, hadi kuandika hili
Ni usia wa mvungi, aliompa Sadali
Wa kilemba au shungi, kila mtu yake hali
Kama wataka haramu, basi kula ilonona

Usifanye kwa kuiga, kuona ndio ufanye
Zitumie zako kuga, mwenyewe na ujikanye
Uoga si wa kufuga, kaa chini jikusanye
Kama wataka haramu, basi kula ilonona

Hatufanani hakika, kwa sura au fikira
Pambana na heka heka, ukomeshe ufukara
Jiondolee mashaka, nenda pasi na papara
Kama wataka haramu, basi kula ilonona

Amua kwa mara moja, pigana na utashinda
Hii vita si ya mmoja, kataa kupindapinda
Usiwe mtu viroja, pambano litakushinda
Kama wataka haramu, basi kula ilonona

Usisikize ya watu, wengi wamejawa husda
Funga kamba za viatu, tembeza hata visoda
Shida zako si za watu, acha wakupake poda
Kama wataka haramu, basi kula ilonona

Abuuabdillah [emoji3578]
0744883353
Jumaomari5@gmail.com jumaomari@ymail.com
 
Yako finyu mawazo, taifa lina hasara
Wafikiri hilo wazo, yatakuwaje madhara?
Rushwa kwenye hizo tozo, mwavimbiwa mnahara
Viondoeni vikwazo, boresheni mazingira

Madaraka mwayapata, mtuletee nafuu
Tuondolee ukata, gharama maisha juu
Ubunifu si utata, uongozi si ndo huu?
Changa vizuri karata, furahia naniliu

Fanya kazi kwa bidii, daima muombe Mungu
Akiba dunia hii, benki siyo kwenye chungu
Iweke sukari chai, tamu iizidi chungu
Maisha walio hai, uwe mwema si mjungu

Hima tutendeni haki, kwa kila mmoja wetu
Kwa mmoja ama laki, kuonea 'sithubutu
Kuumiza usitake, heshima kwa kila mtu
Halali tuneemeke, binadamu sio chatu
 
Back
Top Bottom