Shairi la Simba vs Yanga (29/09/2018)

Shairi la Simba vs Yanga (29/09/2018)

Mjukuu wa Hassan-Juma

Senior Member
Joined
Dec 3, 2022
Posts
123
Reaction score
120
WATANI WANA MAMBO

Jumapili yawadia,Ya watani kuumana
Tamati zitafikia,Zile tambo za Mabwana
Mana tumezisikia,Tokea kitambo sana
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama.


Huku mkongo Zahera, Na kule Mbelgiji
Maombaomba wa hela, Na matajiri wa jiji
Kweli Moro ndo mpira, Uturuki ka kimbiji?
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama.


Huku Juko Murshidi, Kule Kisiki Yondani
Pale Ngasa wa spidi, Huku Erasto Nyoni
Kweli kupata ushindi, Ujipange nje ndani
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama.


Wekundu wakishafungwa, Subira huwa hawana
Hudhani hadi kurogwa, Mwezi wote wa lawama
Matokeo yalipangwa, Mara afukuzwe Djuma
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama.


Jangwani nako vurugu, Wao mabondia khaswa
Wasije beba virungu, Na ni bora kuwaasa
Kwamba amepanga Mungu, Zipo siku utakosa
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama.


Lakini wakishindaga, Meno yote nje nje
Wengine hukumbushaga, Yale ya Aden Rage
Eti mbumbumbu mbumbumbu tu, hata asome Mzumbe
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama.


Kile kikundi cha Ngada, Mpira wa kwetu sie
Vyura zao bodaboda, Hii Shoo ya wenyewe
Hizo tambo za baada, Za ile timu nyingine
Hakika litasimama, Jiji la Darisalama


Mwisho niwatakieni, Furaha yenye amani
Furaha yako moyoni, Isimkwaze jirani
Japo viutanitani, Usiache asilani
HAKIKA LITASIMAMA, JIJI LA DARISALAMA.
FB_IMG_1688628593086.jpg
 
Back
Top Bottom