robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Uchi
Mwili
Naomba uniache mimi,
Bado nazangu nyingi hamu,
Maneno atoa ulimi,
Angalau uone yangu elimu,
Nafsi
Nisikilize wangu mwili,
Ni yangu zamu, nafsi,
Kusitiri wangu uchi,
Nikuepushe na nyingi zohali,
Ni adhama kusimama kusi,
Angali u mbichi,
Lisiwe juto ni jukuu,
Mwili
Zifiche zako dafina,
Naona hazina maana,
Huna hata shukrani,
Kila mlo umekula,
Kila vazi umevaa,
Kila jike tia,
Kila kinywaji umetia
Iko wapi yangu hatia?
Nafsi
Zote hizo kwangu harabu,
Hata ufungue vyote vitabu,
Bado nitalihitaji langu vazi,
Na kwangu liwe azizi,
Awali hadi kaditama,
Ndipo acha zangu lawama,
Kwani mchuma janga,
Nawa kwao hula,
Mwili,
Wataka nini nafsi ili uwe wangu darahani?
Starehe au maskani?
Nafsi
Nahitaji tufute yote mahame,
Mahame ya kiroho na upendo,
Nivalishe niujue wa dhati,
Piga goti nione aliyeniumba,
Shukuru nipate yangu bashasha,
Jali wengine nione wangu utu,
Samehe nitoke gerezani,
Nami nitatulia nyumbani,
Sasa ni vishe langu vazi,
Mwili
Kiza kimeondoka,
Nazo nyingi kufuru
Sasa naiona nuru,
Furaha nayo kudumu,
Zisikie zangu salamu,
Nafsi u wangu wa dhati.
Sitokuacha asilani,
Nikumbatie mchana na usiku,
....
Natamani maoni yako🤗
Mwili
Naomba uniache mimi,
Bado nazangu nyingi hamu,
Maneno atoa ulimi,
Angalau uone yangu elimu,
Nafsi
Nisikilize wangu mwili,
Ni yangu zamu, nafsi,
Kusitiri wangu uchi,
Nikuepushe na nyingi zohali,
Ni adhama kusimama kusi,
Angali u mbichi,
Lisiwe juto ni jukuu,
Mwili
Zifiche zako dafina,
Naona hazina maana,
Huna hata shukrani,
Kila mlo umekula,
Kila vazi umevaa,
Kila jike tia,
Kila kinywaji umetia
Iko wapi yangu hatia?
Nafsi
Zote hizo kwangu harabu,
Hata ufungue vyote vitabu,
Bado nitalihitaji langu vazi,
Na kwangu liwe azizi,
Awali hadi kaditama,
Ndipo acha zangu lawama,
Kwani mchuma janga,
Nawa kwao hula,
Mwili,
Wataka nini nafsi ili uwe wangu darahani?
Starehe au maskani?
Nafsi
Nahitaji tufute yote mahame,
Mahame ya kiroho na upendo,
Nivalishe niujue wa dhati,
Piga goti nione aliyeniumba,
Shukuru nipate yangu bashasha,
Jali wengine nione wangu utu,
Samehe nitoke gerezani,
Nami nitatulia nyumbani,
Sasa ni vishe langu vazi,
Mwili
Kiza kimeondoka,
Nazo nyingi kufuru
Sasa naiona nuru,
Furaha nayo kudumu,
Zisikie zangu salamu,
Nafsi u wangu wa dhati.
Sitokuacha asilani,
Nikumbatie mchana na usiku,
....
Natamani maoni yako🤗