Nazikumbuka beti chache zifuatazo:
SAIDI NYOKA:
Watu wajidanganyao, mbali msiwatafute,
Ni hawa wacheza bao, mikononi wana kete,
Kutwa mlo wao hao, ni kumeza meza mate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.
Waongo na wazandiki, wacheza bao la kete,
kitako hawabanduki, utadhani ni viwete,
Hawalijui riziki, japo nusu ya mkate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.
Nina mtaji husema, kumbe lofa kiokote,
Kwenye bao kainama, hatoki lisimpite,
Huku njaa yamuuma, awaza wapi nipate,
Wacheza bao la kete, waongo na wazandiki.
zingine sikumbuki.........
ANDANENGA:
Saidi usituvunge, kwamba dhambi kubadili,
Michezo tusiipange, kwa majina mbalimbali,
Wewe Nyoka au Kenge, kwako jina la asili?
Zingine sikumbuki.............