Shairi: Mgeni siku ya kwanza

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
1. Mgeni siku ya kwanza,
mpe mchele na panza,
mtilie kifuuni,
mkaribishe mgeni.

2. Mgeni siku ya pili,
Mpe maziwa na samli,
Mahaba yakizidia,
Mzidishie mgeni.

3. Mgeni siku ya tatu,
Nyumbani hamna kitu,
Mna vibaba vitatu,
Pika ule na mgeni.

4. Mgeni siku ya nne,
Mpe jembe akalime,
Akirudi mwagane,
Ende kwao mgeni.

5. Mgeni siku ya tano,
Mwembamba kama shindano,
Nyumbani hauishi mnong’ono,
Atetwa yeye mgeni.

6. Mgeni siku ya sita,
Mkila mkijificha,
Mwingie vipembeni,
Afichwa yeye mgeni.

7. Mgeni siku ya saba,
Si mgeni, ana baa,
Hata moto mapaani,
Ametia yeye mgeni.

8. Mgeni siku ya nane,
"Njoo ndani tuagane,"
Akitokea nje,
"Kwa heri, nenda mgeni."

9. Mgeni siku ya kenda,
Enenda mwana kwenenda,
usirudi nyuma,
usirudi mgeni.

10. Mgeni siku ya kumi
kwa mateke na magumi,
hapana afukuzwaye,
afukuzwa yeye mgeni.
 
Kwani Jf kunae mtu alisoma HKL au KLF 😊
 
Good stuff, thanks for sharing. It brings back good old memories. Unaenda shule na fagio ya chelewa, unakipiga cha ndimu, unarudi unakula ubwabwa na maharage uku ukisikiliza kipindi cha mikingamo RTD.
 
Nilisikia zamani nikijua ni wimbo wa taarabu
 
Imenikumbusha siku (miaka) mingi Sana, hiki kitabu na michoro ya watu kama fimbo vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…