JOTO LA MOTO
JF-Expert Member
- Apr 11, 2018
- 758
- 555
LINAH, LINAH, LINAH
Si kwamba akili sina, zipo ila zimegota.
Nahitaji kukuona, nikome ndoto kuota.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Linah unanivutia, ukweli naweka wazi.
Naikubali hatia, kutamka hivi wazi.
Na ndani mkinitia, sibadili maamuzi.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Nimekaa kufikiri, yupi anifae ndani.
Nataka binti mzuri, aniridhishe moyoni.
Linah we ndo habari, nasema sioni soni.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Linah ninakukubali, sihitaji ushauri.
Nikikuona mahali, moyo utakuwa shwari.
Hebu usikae mbali, njoo utaje mahari.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Nikuonapo pichani, nadata na kila pozi.
Na kunijia kichwani, hisia za lako penzi.
Njoo tuitane hani, itimie yangu njozi.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Linah nakupenda kweli, si kwamba nakutania.
Nipe nionje asali, nipe nitangaze nia.
Hata kama uko mbali, nitazunguka dunia.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Napenda mvuto wako,wa sura na umbo pia.
Hebu nionyeshe kwako, nikuletee rupia.
Nifanye ubavu wako, wakome kunichapia.
Jama nampenda Linah,mleteni nimwambie.
Linah niite ulipo, nije nikukaribie.
Nitakuja mpaka hapo,yenye tamu nikwambie.
Nahitaji hiyo pepo,wachawi niwatambie.
Jama nampenda Linah, muiteni nimwambie..
Nakuwa kama pooza, ninaugua kiwewe.
Nimekufa nimeoza, msababishi ni wewe.
Linah ukinipuuza, nitabadilika jiwe.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Wanasema yupo mtu, eti unaishi nae.
Mwambie asithubutu,nikija anizengue.
Nitakuja na mtutu,kiuno nimtengue.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie
Linah nakusikiliza, majibu unitumie.
Usiache kunijuza, chochote uniambie.
Usije ukanibeza,Linah nitakufa mie.
Jama nampenda Linah,mleteni nimwambie.
Ujumbe ninamaliza,ya moyoni nimesema.
Kwa kweli nimejikaza,kujinusuru mtima.
Na kama nimekukwaza, usiogope kusema.
Jama nampenda Linah, muiteni nimwambie.
Linah Linah Linah, mara tatu nakuita.Si kwamba akili sina, zipo ila zimegota.
Nahitaji kukuona, nikome ndoto kuota.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Linah unanivutia, ukweli naweka wazi.
Naikubali hatia, kutamka hivi wazi.
Na ndani mkinitia, sibadili maamuzi.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Nimekaa kufikiri, yupi anifae ndani.
Nataka binti mzuri, aniridhishe moyoni.
Linah we ndo habari, nasema sioni soni.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Linah ninakukubali, sihitaji ushauri.
Nikikuona mahali, moyo utakuwa shwari.
Hebu usikae mbali, njoo utaje mahari.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Nikuonapo pichani, nadata na kila pozi.
Na kunijia kichwani, hisia za lako penzi.
Njoo tuitane hani, itimie yangu njozi.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Linah nakupenda kweli, si kwamba nakutania.
Nipe nionje asali, nipe nitangaze nia.
Hata kama uko mbali, nitazunguka dunia.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Napenda mvuto wako,wa sura na umbo pia.
Hebu nionyeshe kwako, nikuletee rupia.
Nifanye ubavu wako, wakome kunichapia.
Jama nampenda Linah,mleteni nimwambie.
Linah niite ulipo, nije nikukaribie.
Nitakuja mpaka hapo,yenye tamu nikwambie.
Nahitaji hiyo pepo,wachawi niwatambie.
Jama nampenda Linah, muiteni nimwambie..
Nakuwa kama pooza, ninaugua kiwewe.
Nimekufa nimeoza, msababishi ni wewe.
Linah ukinipuuza, nitabadilika jiwe.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie.
Wanasema yupo mtu, eti unaishi nae.
Mwambie asithubutu,nikija anizengue.
Nitakuja na mtutu,kiuno nimtengue.
Jama nampenda Linah, mleteni nimwambie
Linah nakusikiliza, majibu unitumie.
Usiache kunijuza, chochote uniambie.
Usije ukanibeza,Linah nitakufa mie.
Jama nampenda Linah,mleteni nimwambie.
Ujumbe ninamaliza,ya moyoni nimesema.
Kwa kweli nimejikaza,kujinusuru mtima.
Na kama nimekukwaza, usiogope kusema.
Jama nampenda Linah, muiteni nimwambie.