Kitumba_
Member
- Aug 21, 2018
- 30
- 21
Nianzie kwa salamu, hali zenu kutambua,
Maana ninayo hamu, histori simulia,
Nimifikia hatamu, masomo kumalizia,
Ninachoweza kusema, sasa nimepata kazi.
Jina langu Bilalama, Kitumba ndio mzizi,
Ninatokea Kigoma, ndani ndani kichiizi.
Mtanzania salama, kilimo kwetu jahazi.
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Januari kimakini, kijana nimezaliwa.
Nikaingia shuleni, vitabu kuvibukuwa.
Salama na salmini, vyeti nikatunukiwa.
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Niliacha na kulima, msomi wakaniita.
Ili niweze kusoma, jembe wao kulikita.
Baba pekee na mama, ada waweze ipata.
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Nakumbuka ile- july, mkoa kuukatiza,
Adivansi nika- fly, Kigoma mpaka Mwanza,
Sengerema nili- apply, msuli nikaukaza,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Ardhi university, Oktoba ni kazamia,
Ndani kabisa Dar city, Savei nikatulia,
Uchumi usinipite, hakika nikabobea,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata, kazi.
Sikusahau asili, Balenzi pasi kujali,
Idea nyingi mithili, Profesa kama tayali,
Vichwani kwa kushamili, shule ya kutafakuli,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Siku ile sikulala, dizatesheni timia,
Nikakesha ku-difula, ili tu kumalizia,
Sijamlaumu wala, kwa alivyo nitimua,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Expiriensi nnayo, Mwanza nilijipatia,
LAAC na mengineyo, vyote kushughulikia,
Sivii safi ninayo, rifari kunitetea,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Sina hata la kusema, likija swala la kazi,
Shule nimikwisha tema, ajira watu ni shazi,
Kupigania lazima, utatembea ka chizi,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Sasa nimipata kazi, nautangazia uma,
Nafungua langu zizi, maziwa niweze chuma,
Kuachana na udwanzi, ajira kuisakama,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Kazi nimeyoipata, nikucheza na fursa,
Idea kuzichakata, kama kumla kipusa,
Kipato bila utata, ajira zao pangusa,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Kwa dhati ninayasema, maneno kuweka wazi,
Vumilia Baba Mama, napigana ka nyambizi,
Msingi uje simama, kusaidia wazazi,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Infomesheni zi tele, kuzipata mtandao,
Hapo nitumie shule, usasa muhimu nao,
Nikune kufika kule, ku-change mawazo yao,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Itatunyonya makupe, ajira ughaibuni,
Tutabakia weupe, wala tusiithamini,
Vijana tushike chepe, tukomaeni jamani,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Hapa mwisho nafikiri, kuzishusha zangu tenzi,
Yote mtayanakiri, sijashauri hirizi,
Tutumie kila siri, kuweza ipata kazi,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Maana ninayo hamu, histori simulia,
Nimifikia hatamu, masomo kumalizia,
Ninachoweza kusema, sasa nimepata kazi.
Jina langu Bilalama, Kitumba ndio mzizi,
Ninatokea Kigoma, ndani ndani kichiizi.
Mtanzania salama, kilimo kwetu jahazi.
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Januari kimakini, kijana nimezaliwa.
Nikaingia shuleni, vitabu kuvibukuwa.
Salama na salmini, vyeti nikatunukiwa.
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Niliacha na kulima, msomi wakaniita.
Ili niweze kusoma, jembe wao kulikita.
Baba pekee na mama, ada waweze ipata.
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Nakumbuka ile- july, mkoa kuukatiza,
Adivansi nika- fly, Kigoma mpaka Mwanza,
Sengerema nili- apply, msuli nikaukaza,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Ardhi university, Oktoba ni kazamia,
Ndani kabisa Dar city, Savei nikatulia,
Uchumi usinipite, hakika nikabobea,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata, kazi.
Sikusahau asili, Balenzi pasi kujali,
Idea nyingi mithili, Profesa kama tayali,
Vichwani kwa kushamili, shule ya kutafakuli,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Siku ile sikulala, dizatesheni timia,
Nikakesha ku-difula, ili tu kumalizia,
Sijamlaumu wala, kwa alivyo nitimua,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Expiriensi nnayo, Mwanza nilijipatia,
LAAC na mengineyo, vyote kushughulikia,
Sivii safi ninayo, rifari kunitetea,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Sina hata la kusema, likija swala la kazi,
Shule nimikwisha tema, ajira watu ni shazi,
Kupigania lazima, utatembea ka chizi,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Sasa nimipata kazi, nautangazia uma,
Nafungua langu zizi, maziwa niweze chuma,
Kuachana na udwanzi, ajira kuisakama,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Kazi nimeyoipata, nikucheza na fursa,
Idea kuzichakata, kama kumla kipusa,
Kipato bila utata, ajira zao pangusa,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Kwa dhati ninayasema, maneno kuweka wazi,
Vumilia Baba Mama, napigana ka nyambizi,
Msingi uje simama, kusaidia wazazi,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Infomesheni zi tele, kuzipata mtandao,
Hapo nitumie shule, usasa muhimu nao,
Nikune kufika kule, ku-change mawazo yao,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Itatunyonya makupe, ajira ughaibuni,
Tutabakia weupe, wala tusiithamini,
Vijana tushike chepe, tukomaeni jamani,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.
Hapa mwisho nafikiri, kuzishusha zangu tenzi,
Yote mtayanakiri, sijashauri hirizi,
Tutumie kila siri, kuweza ipata kazi,
Ninachoweza kusema, sasa nimipata kazi.