hapana!Yes Poetic licence BASATA ndio wanatoa!
Nyege kitu asili, anazo na nyungunyungu
Nyege si za akili, katazo ni la mzungu
Nyege zi maadili, hamnazo kwa uvungu
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
Nyege bila kuwepo, singekuwepo uzao
Nyege na yake michepo, zadumu kila uchao
Nyege zi na kicheko, na damu pata ugawo
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
Babio na mamio, wametokana na nyege
Umbulo na amiyo, hawakujengwa kwa zege
Vipi uzungu salio, kututenga degedege?
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
Nyege kunyegezana, kwa wema tukafanana
Twende kugezeana, sema hatutabanana
Vipi leo tunakwama, asili kuhamahama?
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
Andanenga kaanzisha, mimi kuja kumaliza
Nyege nimeidhinisha, ukipata kumaa liza
Si jambo la kirihisha, ukidata unafiza
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
Kalamu naweka chini, nimefika kaditama
Vijijini na mijini, tujitwike baba mama
Kazi yataka makini, uzazi dawamu kama
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
Ha ha ha joking! Poetic licence is like I say the bus growled uphill instead of simply bus went uphill.The player who scored was completely unmarked he was free as a molecule.hapana!
BASATA hawatoi poetic licence!
hata kwanza nawashangaa wanavodhalilisha taaluma yao!
Poetic devices ni uhuru wa msanii kutumia lugha/ sanaa bila kufungwa na kanuni na misingi ya lugha husika!
hahahaha got me!Ha ha ha joking! Poetic licence is like I say the bus growled uphill instead of simply bus went uphill.
Kiranga sende mrama, kaditama sio kiama ,
Kienda si mwanae kwenda, kienda rudi tuanze sema ,
Nani matusi kasema, nayasaka nitoe lana ,
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .
Utusi u kamusini, kwani yalowekwa na nani ?
Ninayo I kamusini , hilo katazo la nini ?
Si wanayo shubakani, hawalioni kwa nini ?
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .
Tulikwenda na shuleni, tukakariri vichwani ,
Mwanagenzi yu huruni, kukunja viriga tungoni ,
Haya kwetu ni mageni, sizo kunga shairini ,
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .
Andanenga na Mloka, sifazo kwao hakika ,
Walitunga yakatundika, na Shabani msifika ,
Wote nao na Soyinka, walijua kuandika ,
Raha ya nyege nyegeni , sheria zilianza lini ????
UrodaJambo baya kbs ni kwamba taasis ya kiswahili Tanzania inajisahau sana, yaan inaacha maneno mengi sana ya kiswahili yatumike kiutusi utusi tu, kuliko yanavyopaswa kutumia kwenye jamii.
Mfano neno kutia..
Kutembea
Mtarimbo
Ngja wa mulize NS maana walipokuwa Burundi walikuwa wanauimba na kuuchezaNyegezi.... where you at?
Mkuu Nyani Ngabu mgambo wako wa BASATA wameshafanya kazi yao kwa diamond na wasafi festival yake.
kashakuambia Andanenga yeye hatukani kamwe "NYEGE KUNYEGEZANA" maana yake "WEMA KUTENDEANA".
Ufafanuzi wa nyege ni kunyegezana katika Kiswahili
nyege ni kunyegezana | Ufafanuzi katika Kiswahili - Oxford Living Dictionaries
MSEMO
- nyege ni kunyegezana
1wema ni mpaka uwe wa kutendeana.
Maana yake, wema wa kufanywa upande mmoja tu, si wema, ni unyonyaji na utumwa.
Kwa kweli "Nyege ni kunyegezana" ni msemo wa Kiswahili uliokuwepo miaka mingi kabla Amiri Akida "Sauti ya Kiza" Andanenga hajaandika shairi la jina hilo.Maana yake, gwiji wetu Andanenga hakujizushia tu kuandika shairi hilo, bila muongozo, alilitoa katika misemo ya Kiswahili.
Halafu msemo wa "Nyege ni kunyegezana" ni msemo mrefu sana, hata neno lenyewe "nyege" limekuwa over sexualized.Kwa tunaojua Kiswahili cha ndani, nyege ni tamaa fulani hivi, si lazima hata iwe ya sex.Yani ni hamu kubwa, mtu kusema "nina nyege na movie ya action leo" ni kitu cha kumaanisha nina hamu ya kuangalia movie ya action, nothing sexual.
Kwahiyo huo msemo wa "Nyege ni kunyegezana" ulivyokuwepo zama na zama, unaweza kuwa mpana sana, kumaanisha.
Kimsingi, msemo unasisitiza reciprocity and propagation
1. Habari ni kupashana
2. Mapenzi ni kupendana
3. Kazi ni kushirikiana
4. Familia ni kuzaliana
5.Shughuli ni kukaribishana
6. Chakula ni kugawana
7.Heshima ni kuheshimiana
9. Uzuri ni kukubaliana
10. Vicoba ni kukopeshana