Shairi: Shati la rangi

Shairi: Shati la rangi

Mbavu mbili

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
1,457
Reaction score
874
SHATI LA RANGI

Mgonjwa mwenzi kitanda,nafsi yanikumbukiza
Wa miongo na si kinda,maovu yanichukiza
Ukweli nitautenda,sitoita muujiza
Navua shati la rangi, silitaki lina damu


Weledi wanisikia,mamba huishi majini
Si yakale nasimulia,wajitoa hatarini
Tegoni walikalia,machuta vichwa chini
Navua shati la rangi,silitaki lina damu


Wachache wawasadiki,imani wamejivua
Imejawa wazandiki,hakuna wa kunasua
Porojo na unafiki,dini yao twaijua
Navua shati la rangi,silitaki lina damu


Upepo hauna dawa,kukinga wajisumbua
Usimfadhili chawa,damu ataitumbua
Kutowaamini dawa,mapema kuwapembua
Navua shati la rangi,silitaki lina damu


Ukijivua viatu,mibani waweza pita
Adui ni mbwa mwitu,pinga na utamkita
Kicheko chao cha kutu, cha kale na kimepita
Navua shati la rangi,silitaki lina damu


Tungo ya sita yatua,makenu nayaanika
Joka ninalirarua,mdomo linaanika
Nalitosa kulijua,upole likijivika
Nalivua shati la rangi,silitaki lina damu
 
Ni shati ama ni gamba, ulivualo wakwetu?
Ni wengi wavua gamba, utadhania ni chatu
Rudia humu kugamba, kijiweni hapa kwetu
Nakuhisia wakwetu, ulivualo ni gamba!

Kama lako ni la mamba, halivuliki wakwetu!
Jibu lisiwe la pumba, jibu moja si matatu
Tujibu bila kutamba, pia tena na kwa utu
Nakuhisia wakwetu, ulivualo ni gamba!

Si joho bali ni gamba, kama hao wengi wetu
Siyo shati bali gamba, na roho zenu za kutu!
Vua koti hata gamba, jibadilishe na utu
Nakuhisia wakwetu, ulivualo ni gamba!
 
Hahahahahahahahahahahahahahahaha...hehehehehehehehehehehehe...hihihihihihihihihihihihihihihi...hohohohohohohohohohohohoho...kumbe ni chichiemu!
 
Back
Top Bottom