Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
SHAIRI: SUMU YA UKALE VICHWANI MWETU
MTUNZI: MULIKUZA PASCHAL
Mkataa kwao kweli mtumwa,
Na mcheza kwao daima hutunzwa,
Daima tupende asili yetu kama paka na maziwa,
Tukivikimbia vyetu mwishowe tutakuja kulaumiwa.
Mababu zetu daima tunawaenzi milele,
Wapendao vya jirani daima hatutachoka kuwapigia kelele,
Mtakuwa watumwa na kuendeshwa kama misukule,
Yahitajika wenu utashi wazazi kuwapa vijana shule.
Lakini lenye mwanzo daima lina mwisho,
Wakale walipenda ukeketaji sasa ni michosho,
Yapelekea vifo vingi mpaka inatupa tisho,
Makabila mpendayo kufanya hivyo daima hamtapata posho.
Wengine tunawaogopa kuwakaribisha makwetu,
Mambo ya giza mwayashikilia mwishowe mje mtuchanjie wanetu,
Foleni kutwa kupeleka kuku kwa sangoma mkidai ndiyo jadi yetu,
Mahospitalini kutia mguu mmekuwa wagumu mkiendekeza huko tu.
Bado wengi mwaendelea kurithi wajane mkidhani ni ustadi,
Jamani huo ni ulimbukeni nasiyo zetu tena jadi,
Kukaribisha magonjwa kwa zenu nyingi juhudi,
Wenu mshauri nikitaka mbadilike nipo mlangoni nikibisha hodi.
Ngoma ngomani wengi mwazipenda,
Sasa wengi mwazicheza na kanga moja uzinzi mwaupanda,
Mwazicheza kwa lengo la kupata pesa na wengi wanawapenda,
Zenu ngoma za vichochoroni jamani naziponda.
Na mnaozalishiwa majumbani msione ufahari,
Wengine waozesha wao vitoto wakitaka ng’ombe waonekanike majemedari,
Jamani jalini utu wenu na wa wenzenu msilete kimbari,
Mshikiliao ukale badilikeni kwani elimu ni bahari.