Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
Penzi lako nili tamu,kwako nipo taabani
Penzi aliishi hamu, limeingia damuni
Hii sasa yangu zamu, kufurahi Duniani
Nimeipata bahati, kupendwa na Malaika.
Penzi lako kama nuru, linanitoa gizani
Kukusifu si kufuru,wewe ndo wangu mwandani
Nitaanza kufuturu, kupiga vitu fulani
Utamu wa penzi lako, limenitia wazimu.
Usije kunikimbia,nitaenda kilingeni
Uchawi kukufanyia, nikutupie majini
Mganga nitamwambia, akugeuze kunguni
Nipende nitakupenda, ukinacha nakuloga.
Mtunzi: Idd Ninga
Penzi aliishi hamu, limeingia damuni
Hii sasa yangu zamu, kufurahi Duniani
Nimeipata bahati, kupendwa na Malaika.
Penzi lako kama nuru, linanitoa gizani
Kukusifu si kufuru,wewe ndo wangu mwandani
Nitaanza kufuturu, kupiga vitu fulani
Utamu wa penzi lako, limenitia wazimu.
Usije kunikimbia,nitaenda kilingeni
Uchawi kukufanyia, nikutupie majini
Mganga nitamwambia, akugeuze kunguni
Nipende nitakupenda, ukinacha nakuloga.
Mtunzi: Idd Ninga