SHAJARA YA MWANA MZIZIMA 3 Abdallah Tambaza

SHAJARA YA MWANA MZIZIMA 3 Abdallah Tambaza

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SHAJARA YA MWANA MZIZIMA 3
Abdallah Tambaza

Kitabu kipya katika mfululizo wa Shajara ya Mwana Mzizima kimetoka.

Mfululizo wa vitabu hivi umefanikiwa kuhifadhi historia ya Dar es Salaam ambayo si watu wengi wanaijua kwa kina.

Katika kitabu hiki kipya nimevutiwa sana na jalada la kitabu ambalo linamuonyesha Mwalimu Nyerere akiwa viwanja vya Ukumbi wa Karimjee kabebwa mabegani mwa wanachama wa TANU.

Mbele kabisa katika picha yuko mama yake Nyerere Bi. Mugaya Nyang'ombe na pembeni yake yuko Sheikh Issa Nasir wa Bagamoyo na nyuma yake yuko Oscar Kambona.

Pembeni kwa Mwalimu Nyerere chini yake yuko Rajab Diwani fundi seremala aliyeacha randa baada ya TANU kuundwa 1954 na kujitupa katika harakati za ukombozi wa Tanganyika.

Picha hii ni siku ambayo Waziri wa Makoloni Iain Macleod alipotoa tarehe ya uhuru wa Tanganyika.
Mwanzo wa kitabu hiki mwandishi anaeleza maana ya uhuru na yale yaliyowafanya Watanganyika wadai uhuru wao.

Naamini sura hii ya kwanza ndiyo iliyofanya kitabu hiki kiwe na picha ya Mwalimu Nyerere kashika bango linalonadi tarehe ya uhuru.

Kitabu hiki mwandishi katayarisha mapishi tofauti sana na yale wasomaji wake tumeyazoea kuanzia historia ya Saba Saba siku TANU ilipoasisiwa, maisha ya Aluta Amri Abeid, Saadan Abdu Kandoro, Shaaban Robert hawa wakiwa watu maarufu katika miaka ya 1950 wakati wa kupigania uhuru.

Mwandishi anaeleza ndani ya kitabu maisha ya watu maarufu wa miaka ya karibuni kama Sunday Manara, Reginald Mengi hadi kufika kwa Sheikh Zuberi Yahya, hawa wawili Mengi na Sheikh Zuberi wakiwa marehemu.

Hiki si kitabu cha kukosa.
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani bei shs: 10,000.00.
SHAJARA 3.jpg
 
Maalim Mohamed Said Abdallah Tambaza ndiye Jumbe mwenyewe au huyu mtoto wake?

Jirani zetu kitambo sana Upanga hawa kina Tambaza.
 
Back
Top Bottom