Shaka amezitaka taasisi za umma zenye miradi mikubwa ya maendeleo kuwa na bajeti maalum ya kuhudumia miradi hiyo

Shaka amezitaka taasisi za umma zenye miradi mikubwa ya maendeleo kuwa na bajeti maalum ya kuhudumia miradi hiyo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM taifa Shaka Hamdu Shaka amezitaka taasisi za umma zenye miradi mikubwa ya maendeleo kuwa na bajeti maalum ya kuhudumia miradi hiyo.

Shaka alisema hayo leo wakati alipotembelea hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara mjini Babati.

“Nitoe wito kuwe na bajeti maalum ya kuhudumia miradi hii yenye thamani kubwa ili kuilinda” alisema.

alisema hayo baada ya kutembelea mtambo wa kuzalisha gesi hospitalini hapo ambapo aliambiwa kuna changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na udhaifu wa jengo, kukatikakatika kwa umeme kulikosababisha baadhi ya vifaa vya mtambo huo kuungua.

“Wizara husika zihakikishe zinajenga majengo yanayoendana na hadhi ya mitambo” aliongeza Shaka ambaye yuko katika ziara ya kujitambulisha kama mlezi wa chama wa mkoa huo.

Ameipongeza serikali ya Rais Samia kwa kutekeleza kivitendo ilani ya uchaguzi ya CCM katika eneo la afya.

“Tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi.. ukisoma ilani ya uchaguzi kifungu G ibara ya 83 inaeleza kuimarisha hospitali 28 nchini kuwa za rufaa na Hii ni miongoni mwao “ alisema.

Mwisho

IMG-20220515-WA0560.jpg

IMG-20220515-WA0558.jpg

IMG-20220515-WA0557.jpg

IMG-20220515-WA0556.jpg

IMG-20220515-WA0555.jpg

IMG-20220515-WA0561.jpg
 
Back
Top Bottom