Shaka amkabidhi Sophia Mjema ofisi ya Itikadi na Uenezi

Shaka amkabidhi Sophia Mjema ofisi ya Itikadi na Uenezi

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Makabidhiano yamefanyika Lumumba.

Hongera shaka kwa kukabidhi ofisi kwa amani, zinazofuata ni picha za makabidhiano ya ofisi.

IMG_1162.jpg

Hapo ndugu Shaka akitabasamu kwa bashasha bila tashwishwi.
 
Kashiba pesa sasa anasubiri kwenda chooni kupunguza alichokula na kuvimbewa
 
IMG-20230122-WA0032.jpg
Aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, amemkabidhi ofisini Sophia Mjema.

Shaka, amemkabidhi ofisi ikiwa ni siku chache baada ya Mkutano Maalum wa Halmashauri Kuu ya CCM, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Mjema kuchukua nafasi ya Shaka.

Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, Dar es Salaam.
 
Hadi mkuu wa mkoa ndio katokea huko baada ya kutoka ilala kama mkuu wa wilaya.
Ukuu wa Wilaya alitemwa baada ya kuingia kwenye mbio za ubunge Ilala. Kakaa sana kitaa, kakumbukwa na mama baada ya kuyashika madaraka.
 
Ukuu wa Wilaya alitemwa baada ya kuingia kwenye mbio za ubunge Ilala. Kakaa sana kitaa, kakumbukwa na mama baada ya kuyashika madaraka.
Baada ya kukosa ubunge aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga, uenezi katokea Shinyanga kama mkuu wa mkoa.
 
Hamidu Shaka kazira hadi kuvaa nguo za CCM kwenye makabidhiano kweli kachukia kuondolewa

Mavazi aliyovaa kwenye makabidhiano yanaongea mengi
 
Nilikua namkubali Hamdu Shaka, sijui kama alikua na makandokando yake.
 
Hamidu Shaka kazira hadi kuvaa nguo za CCM kwenye makabidhiano kweli kachukia kuondolewa

Mavazi aliyovaa kwenye makabidhiano yanaongea mengi
Alishaonywa sana humu mitandaoni.
Kusifu na kuabudi mtu kisiasa siyo sera ya chama.
 
Hamidu Shaka kazira hadi kuvaa nguo za CCM kwenye makabidhiano kweli kachukia kuondolewa

Mavazi aliyovaa kwenye makabidhiano yanaongea mengi
Tuli mwambia hakusikia!
 
Back
Top Bottom