Shaka Hamdu Shaka ataka walioisababishia Serikali hasara ya TZS 0.59BL watafutwe

Shaka Hamdu Shaka ataka walioisababishia Serikali hasara ya TZS 0.59BL watafutwe

Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka ameitaka Serikali Wilayani ya Bukoba kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wataalamu na wakandarasi waliohusika kuisababishia hasara Serikali ya milioni 590 kwa kutekeleza mradi wa maji wa Katale uliopo tarafa ya Bugabo.

Akiwa katika Ziara ya Sekretarieti ya CCM-Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg Daniel Chongolo amesema mradi huo wa Katale uliopo halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ulitekelezwa chini ya kampuni ya ujenzi ya STC ambao hata hivyo hautoi maji miaka miwili tangu kukamilika kwake na kukabidhiwa.

Mjomba fanya kazi
 
Back
Top Bottom