Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wachambuzi mbali mbali wa kivita akiwemo raisi wa Ufaransa wamesema lengo la Israel kuifuta Hamas ni miongoni mwa malengo dhaifu ya vita vinavyoendelea Gaza.
Raisi huyo baada ya kushuhudia hali ya vita inavyojikokota amesema wakati umefika kwa mamlaka ya Israel kutoa maelezo ya wazi kuhusu vita hivi.Kwani iwapo lengo ni kuifuta Hamas basi itachukua hata miaka 10
Naye mchambuzi wa kipalestina Tahani Moustafa amesema kufikiria kuifuta Hamas ni ndoto za mchana kwani Hamas imeingia kwenye fikra ya kila mmoja kuwa inapigania ardhi za wapalestina ambazo zinakaliwa na Israel.Fikra hiyo haiwezi kufutika kabisa kwa kuzingatia kile kinachoonekana.
Naye Michael Milshtein ambaye ni afisa usalama wa Israel wa zamani amesema dhana ya kuishinda Hamas ni dhana isiyoeleweka vyema hasa ukiangalia kuwa kila siku ndio tunashuhudia mapigano makali zaidi
Meja Generali mstaafu,Giora Eiland kwa upande wake amesema kuuliwa kwa makamanda wa Hamas hakukuanza leo na haijawahi kusababisha kudhoofika kwa kundi hilo.Wana uwezo wa kuingiza makamanda wengine kwa haraka na ambao wanakuwa wakali kuliko watangulizi wao.