Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Majuzi hapa tumemsikia katibu wa propaganda wa CCM akijimwambafy kuhusu uimarishwaji wa kila sekta nchini kupitia serikali ya CCM.
Ameenda mbali zaidi kutuita sisi wakosoaji kama.maadui wa mama na tunamtakia mabaya hivyo azibe masikio achape kazi aachane na sisi wanafiki.
Katika posti zangu nyingi nimekosoa kasumba ya wanasiasa na wahuni serikalini kuwa wanawahadaa wananchi kuwa pesa za maendeleo zinatolewa na Rais. Pesa ya umma inatolewa kwa utaratibu uliopitishwa na Bunge kupitia sheria ya fedha ya mwaka wa fedha. Lakini wanaendelea kujikaanga kwa kusema.uongo mtukuka mbele ya umma.
Tukio la ajali ya ndege pale Bukoba limeleta uwiano na picha halisi ya hali ya nchi kiuchumi, kisayansi na kijamii. Nchi ina ufinyu wa mikakati na mipango endapo kutatokea majanga na dharura.
Shaka, tumia nafasi yako kusimamia na kufuatilia utekelezwaji wa ilani na kisha pokea malalamiko ya wananchi na kuyawasilisha kwenye vikao vya chama ili kulenga upatikanaji wa suluhu za changamoto hizo.
Mezani kwako kuna taarifa lukuki za malalamiko ya wananchi lakini kutwa kuchwa upo bize na ziara za kuwapiga mikwara wakosoaji wa chama. Wananchi ndiyo wanaotumika (si tunaiba kura bana) kuiweka CCM madarakani. Nasema wanatumika kwa sababu tumeweka sheria kali hakuna kuhoji matokeo ya urais mahakamani... tume imeajiri wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wakuu wa chaguzi katika wilaya zao....
Nilisema, na nitaendelea kusema kuwa kila uongo ambao CCM inawahada wananchi umefikia kikomo. Mtatuua lakini ukweli utabakia kwamba CCM soon itawekwa pembeni ili ijifunze namna ya kuishi kwenye imani ilizojiwekea yenyewe (kumbuka imani za Mwana TANU)
Aibu yetu

- Tunaishi kwa kudra za Rais kwa sababu hajatoa hela za kununulia vifaa vya uokozi katika majanga mbalimbali.
- Rais hajatoa hela ya kuajiri wataalam wa kutosha kwenye uokozi na majanga ambayo.hatuna miadi nayo
- Rais hajatoa pesa ya kujenga uzio wa viwanja vya ndege
- Rais hajatoa fedha kuwezesha elimu kwa umma hasa katika sekta ya uokozi na dharura mbalimbali
- Rais hajatoa hela kwenye ununuzi wa boti za dharura kwenye viwanja vya ndege vilivyo jirani na ziwani aua baharini