Huyu Shaka Namuona mbali Sana kiuongozi, Anapaswa kupanda na kupandishwa juu zaidi ya hapo Alipo, Anapaswa kuaminiwa katika nafasi za juu zaidi kiuongozi zitakazo mpa mamlaka ya kuwawajibisha watu, Anapaswa kuongezewa nguvu za kimamlaka kwa kuwa Ni kijana aliyeonyesha kuwa na uchungu na Rasilimali za nchi hii, Ni kiongozi aliyeonyesha kuumizwa na matatizo ya watanzania.
Ni kiongozi mwenye kiu ya kuona watanzania wanapata Milo mitatu kila Siku, Ni kiongozi mwenye uchu wa maendeleo, Ni kiongozi mwenye utulivu,busara, upendo, unyenyekevu, uvumilivu hekima na huruma kwa watu, Ni kiongozi anayetambua kuwa cheo Ni dhamana,Ni kiongozi asiye na majivuno ya kiuongozi, Nikiongozi asiye na ulevi wa kimadaraka,
Kwake Shaka uongozi Ni utumishi kwa watu na siyo kutumikiwa na kuumiza watu, kwake Shaka uongozi Ni kusaidia watu na siyo kuwa didimiza na kuwaonea,Shaka ana uchungu mkubwa na uzalendo mkubwa na nchi hii,
Nampongeza Sana mama Samia suluhu Hassani Mwenyekiti wetu Taifa kutuletea kiongozi huyu mwenye Maono na uzalendo mkubwa kwa Taifa letu, Hakika Timu ya uongozi ya CCM Taifa Ni timu iliyosheheni wazalendo watupu ambao wamekuwa mfano wa kuigwa kwetu wanachama wa kawaida
Kazi iendeleee