Shakahola: Macho yote Mahakamani Mombasa, Mackenzie na wenzake kuhukumiwa leo Katika Kesi ya Vifo 191

Shakahola: Macho yote Mahakamani Mombasa, Mackenzie na wenzake kuhukumiwa leo Katika Kesi ya Vifo 191

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38

​
Macho ya Wakenya yanaelekezwa katika Mahakama ya Mombasa, ambapo mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie na washirika wake wanatarajiwa kusomewa hukumu katika kesi inayohusishwa na vifo vya watu 191, wengi wao wakiwa watoto, katika mkasa wa Shakahola.

Mackenzie, aliyejitambulisha kama mhubiri, anakabiliwa na mashtaka ya mauaji pamoja na washukiwa wenzake. Upande wa mashtaka unadai kuwa wafuasi wa dhehebu lake walihamasishwa kufunga kula ili, kwa madai yao, kukutana na Yesu.

Kesi hiyo imevuta hisia za taifa kutokana na ukubwa wa mkasa huo na maswali mazito kuhusu usimamizi wa shughuli za kidini, ulinzi wa watoto na hatua zilizochukuliwa na mamlaka kuzuia vifo hivyo.

Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa mashahidi 121, huku mahakama ikiamua mwezi Aprili 2026 kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwataka washtakiwa wajitetee. Hata hivyo, uamuzi huo wa awali haukuwa hukumu ya hatia.

Hukumu inayotarajiwa leo inaweza kuwa hatua muhimu katika kesi hiyo iliyofuatiliwa kwa karibu na umma.

Je, kesi ya Shakahola imeonyesha kuwa Kenya inahitaji usimamizi mkali zaidi wa taasisi za kidini ili kuwalinda waumini dhidi ya viongozi wanaoweza kutumia vibaya imani yao?
 
Na yeye akae bila kula mpaka afe
Tatizo la jirani wana Uhuru sana upande wa dini zao.
Kuna mmoja aliwaaga waumini wake kuwa anapaa Baada ya kupanda mti
Waumini wakiwa chini wakimuangalia apae
Alipofika juu kabisa huku matawi yakiwa madogo aka pause kwanza na camera zikawa off
Jirani watamalizia mkasa sisi hatujui
 
Hana kosa lolote. Ni ujinga wa wahanga wenyewe.
Itabidi hata sadaka wasitoe makanisani maana huwa wanashawishiwa kama ilivotokea ndio maana wengine wanatoa vyote na kubaki hamna kitu njaa zikiwaua si ni kesi ileile?
 
Nakumbuka hii kesi ila inamaana hao wote walikuwa wanapata faida gani na kuuwa watu hao?

Cult au?
 
Back
Top Bottom