Shamba langu. Bustani ya ndoto zangu

Shamba langu. Bustani ya ndoto zangu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Je wajua ya kwamba ndoto zaweza kuwa kweli? Wazungu wanasema dreams can come true...

Fanya yote maishani.. Pambana sana lakini usiache kumwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema zote akujaalie mwisho mwema, uzee uliojaa fanaka na baraka.. Tele.. Wanazengo wanasema fainali uzeeni.. Basi Mwombe sana Manani akutunuku fainali ya ushindi.. Sio ya kutoa suluhu wala kufungwa..!

Pamoja na yote utakayojaaliwa pata walau hekari moja ukikosa kabisa basi walau nusu yake .. Kishapo
Jenga kajumba kako kazuri sana.. Huhitaji ghorofa wala nyumba kubwa utafuga majini na mashetani bila

kutaka na bila kujua
Fuga mifugo yako michache
1. Ng'ombe wa maziwa mmoja wakizidi wawili
2. Kuku wawili watatu wa mayai wa kienyeji
3. Ukiweza na ukipenda fuga na bata au sungura
4. Bwawa dogo la samaki
5. Fuga njiwa ukiweza na kasuku na ndege wengine wa leisure
Hii mifugo yote
Hawa wote watakusaidia sana kwenye ishu ya mbole
Kuzunguka nyumba una bustani zako za maua, garden na miti ya vivuli
Huko shambani sasa unatenga eneo la shamba dogo mazao mixer miti ya matunda.. Eneo lililobaki bustani za mbogamboga..
Utahitaji kisima pia
Pengine utahitaji vijana wawili watatu wa kukusaidia
Utahitaji chumba/ghala lenye vitendea kazi vyote...
Eat well.. Eat fresh.. Na kamnywesho kidogo😀😀😀
1741281608522.jpg
1741281594746.jpg
1741281605227.jpg
1741281041286.jpg
 
Na maisha yanakuwa mazuri kabisa hata usipojenga na kuviweka karibu na unapoishi basi viwepo sehemu ambayo ukihitaji kufika unaweza kufika kila siku na ukafurahia maisha .

Ukweli ni kuwa ndiyo maisha yenye amani na furaha na ikiwa umejaaliwa kuwa navyo katika umri ambao bado umri haujaanza kukukataa🙏🙏
 
Back
Top Bottom