Shamba linauzwa Vikindu

Mchanya

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
997
Reaction score
1,568
Shamba la ekari kumi (10) au zaidi linauzwa eneo la Vianzi, ni umbali wa Km 6 kutokea Vikindu, barabara ya Kilwa, Km 36 kutokea katikati ya jiji la Dar. Linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji, kwa mazao ya mbogamboga na matunda, ufugaji na hata kwa mradi ya muda mrefu. Shamba linafikika kwa gari. Bei ni Tshs; M4 kwa ekari moja. Piga 0784 607524 kwa maelezo zaidi.
 
Sehemu gani hapo vikindu? Upande wa Kazole? Au wapi?
 
Huwezi ukawa serious.... heka moja milioni 4???????? Yaani sqm 4046 unaziuza milioni 4??????

Kuna jamaa kauza heka moja mil 15.... tena hapo kwa kuwa alikuwa na shida ya haraka. (Maana hata ukikata vipande vya 20 kwa 20 ukiuza kwa bei ya kutupa mil 2 kwa kipande heka moja utapata almost vipande 10 ambavyo ni mil 20 kwa hekari.....

(Unless hilo shamba lipo mbali na halifikiki au bondeni)

Review bei yako mkubwa... (samahani nimeongea mengi yasiyohusiana na ununuzi)
 
Shamba liko Vianzi (Majumba Sita) ni umbali wa kilometa sita (6) kutokea Vikindu barabara ya lami
 
Unamdanganya mwenzio, atakaenunua milioni 15 eka 1 hilo eneo ni chizi, bei ya ardhi upande huo ni milion 3 kwa eka.
 
Unamdanganya mwenzio, atakaenunua milioni 15 eka 1 hilo eneo ni chizi, bei ya ardhi upande huo ni milion 3 kwa eka.
Kama huna hiyo hela lazima uone unadanganywa. Unajua ukubwa wa ekari moja??????? Na kumbuka hawa hawauzi ekari moja bali almost ekari moja na robo (m70 kwa 70)

Plus eneo na jinsi palivyo
 
Kama huna hiyo hela lazima uone unadanganywa. Unajua ukubwa wa ekari moja??????? Na kumbuka hawa hawauzi ekari moja bali almost ekari moja na robo (m70 kwa 70)

Plus eneo na jinsi palivyo
Wewe na huyo mtoa Tangazo wote ni mtu mmoja, tumeshtukia. Haumpigi mtu hapa..
 
Wewe na huyo mtoa Tangazo wote ni mtu mmoja, tumeshtukia. Haumpigi mtu hapa..

Akili zako ndipo zilipoishia.

Umekosa hoja umeamua kutoa shutuma.

Kwaheri.

(Anyway........ inawezekana pia wewe na huyo mtoa mada lenu moja sasa unaona nimekuharibia)
 
Kama barabara ya lami kwa nini mnauza bei ya kutupa????? Kama eneo ni nzuri sio bonde hapana mgogoro wala tatizo...... kwa nini usilikate vipande....ungepata zaidi kuliko kuuza eka mil 4

Ingawa ingekuwa mimi nisingeuza mpaka angalau miaka 2 mbele maana ardhi ina-appreciate.... na vikindu patakua keki karibuni (samahani nimekupa ishauri badala yake)

Shamba liko Vianzi (Majumba Sita) ni umbali wa kilometa sita (6) kutokea Vikindu barabara ya lami
 
Mkuu km 6 kutoka kwenye lami bado unasema barabara ya lami? Lakini kwa serikali hii hizi bei za kukuza kuza za viwanja zitatoweka....watu wamezoea kununua kwa bei kubwa kwa sababu ya wizi wizi na madili dili tu ... sasa mihanya yote itatiwa kufuli, heshima inarudi mtaani....pesa inakuwa na dhamani.!
 
Hapo kwenye km sikumsoma vizuri.

Ila ukiangalia kwa bei ya serikali usidhani kama kuna unafuu maana kwa sasa sqm 1 inarange kati ya 8,000 hadi 10,000 inategemea makazi au makazi na biashara. Kwa hiyo ekari moja 10,000×4046 = 40,460,000!!!!! Wenzangu na mie lazima tuishie sqm400

Ila bora serikali ikaja na mpango wa kupima viwanja na kuhakikisha vinapatikana kwa bei resonable..... kuepuka kuvunjiana baadae au ndio unanunua unakuta limepangiwa kuwa open space

Mkuu kama upo hai nakushukuru sanaa
2015 baada ya kuona huu uzi nilienda kununua eneo mita 30*25 elfu 30
Vikindu-kazole-komakoma january 2024 nimeenda hakika elfu 30 yangu ilienda sawa kabisa
 
Kwa sasa huo ukubwa unanunua kwa bei gani?
Mkuu kama upo hai nakushukuru sanaa
2015 baada ya kuona huu uzi nilienda kununua eneo mita 30*25 elfu 30
Vikindu-kazole-komakoma january 2024 nimeenda hakika elfu 30 yangu ilienda sawa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…