Shambulio la DusitD2: Je Kenya ina uwezo wa kuwazuia wapiganaji wa al-Shabab kutoka Somalia ?

Shambulio la DusitD2: Je Kenya ina uwezo wa kuwazuia wapiganaji wa al-Shabab kutoka Somalia ?

BuletAngle

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2017
Posts
688
Reaction score
556
_105218905_f8c767d6-859e-400d-bdcd-e962d63aa357.jpg


Shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa Kisomali jijini Nairobi tarehe 15 Januari ni mapinduzi makubwa ya Propaganda kwa upande wa wapiganaji hao na kusisitiza wasiwasi kuhusu uwezo wa Kenya kukabiliana na ugaidi.

Wapiganaji hao walitumia vilipuzi na risasi kuingia katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 na ofisi nyengine zilizopo katika eneo la Riverside Drive 14 katika eneo la Westlands, karibu na duka la jumla la West Gate Mall ambalo lilishambuliwa 2013.

Rais Uhuru Kenyatta alisema mnamo tarehe 16 Januari kwamba watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na kwamba magaidi wote waliangamizwa.
Kanda za kamera za CCTV zilizopeperushwa hewani na vyombo vya habari viliwaonyesha watu wanne waliokuwa wamevalia magwanda meusi wakifyatua risasi za rashasha walipokuwa wakiingia katika hoteli hiyo.

umbukumbu za West Gate.K
Kundi la Al-Qaeda linalohusiana na wapiganaji wa al-Shabab waliodai kutekeleza shambulio la Westgate Mall ambapo takriban watu 67walifariki walidai kutekeleza shambulio hilo.
Wamedai kuwaua watu 47.

Shambulio hilo lilitokea siku moja baada ya mahakama ya Nairobi kuwashtaki watu watatu kwa mashtaka ya kuwasaidia al-Shabab kutekeleza shambulio la West gate.
Hoteli ya DusitD2 inarudisha kumbukumbu ya uwezo wa al-Shabab kushambulia ndani ya Kenya, kinyume na madai ya serikali kwamba wanajihad hao wamezuiliwa katika maeneo ya mpakani na Somalia.

Nchini Somalia , kundi la al-Shabab linasalia kuwa tishio kubwa la usalama licha ya operesheni za hivi majuzi za kijeshi na mashambulio ya angani yaliotekelezwa na vikosi vya usalama, wanajeshi wa Muungano wa Afrika AU na vikosi vya Marekani.
Kundi hilo la Kijihad linadhibiti maeneo mengi ya Somali ya kati pamoja na kusini.

Kwa nnii Kenya inalengwa?
Al-Shabab iliimarisha mashambulio yake nchini Kenya wakati serikali ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia kukabiliana na kundi hilo 2011.
Wapiganaji hao waliitaka Kenya kuondoka nchini humo na kuapa kulipiza kisasi.
Wito wa serikali kuondoa wanajeshi wake nchini Somalia umekandamizwa na madai kwamba ujumbe huo una wajibu wa kizalendo.
Wengine wamesema kuwa kuondoka kwa wanajeshi wa Kenya nchini Somalia ni sawa na ushindi wa al-shabab.
Mamia ya wanajeshi wa Kenya wameuawa na wapiganaji wa Alshabab nchini Somalia katika kipindi cha miaka minane iliopita.
Serikali imetetea uwepo wa wanajeshi wake nchini Somalia licha ya wito wa mara kwa mara wa kutaka kuondoka kwa mpangilio, ambao baadhi ya wanaharakati wanasema haufanyiki.

Mpaka wa Kenya na Somalia.
Kenya inagawana mpaka mrefu na wenye mwanya mkubwa na Somalia. Taifa hilo lililopo katika upembe wa Afrika limekosa uthabiti tangu rais Siad Barre aondolewe madarakani 1991.
Mwaka 2017, serikali ya kenya imesema kuwa itajenga ukuta katika mpaka na Somalia ili kuwazuia wapiganaji kuingia nchini.

Ujenzi wa ukuta huo wenye kilomita 700 ulisitishwa mnamo mwezi Machi 2018 kufuatia mgogoro kati ya Wakenya na Wasomalia wanaoishi katika eneo hilo.
Alshabab limekiri kutekeleza baadhi ya mashambulio ya kiwango cha chini nchini Kenya , ijapokuwa baadhi yao huenda yalitekelezwa na baadhi ya makundi ambayo hayashirikiani na kundi hilo lakini yanafuata itikadi yao.

Tangu kisa cha West gate Mall, al-Shabab limetekeleza shambulio moja katika taifa hilo na mengine ya viwango vya chini katika maeneo ya kaskazini mashariki na maeneo ya pwani karibu na mpaka na Somalia.
Mnamo mwezi Aprili 2 2015, kundi hilo liliwaua watu 148 , wengi wao wakiwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Garissa katika eneo la Kaskazini mashariki.

_105218907_c353f7a7-3de7-4433-8b84-5746576643e3.jpg


Athari za shambulio la DusitD2
Shambulio hilo litapiga jeki propangada ya kundi la al-Shabab nchini Somalia pamoja na mataifa ya Afrika mashariki yanayochangia wanajeshi wake katika vita dhidi ya ugaidi.
Wapiganaji hao watalitumia shambulio hilo kuonyesha uwezo wao kushambulia nchini Kenya hususan maeneo yanayotembelewa mara kwa mara na wageni pamoja na maafisa wa serikali.
Pia wana uwezo wa kutumia shambulio hilo kuonyesha uwezo wao mbele ya makundi mengine yanayotii kundi la Islamic State.

Kutakuwa na wito nchini Kenya wa kuimarishwa kwa usalama katika majumba kadhaa na hususan maduka ya jumla ambayo huenda yakapoteza biashara.
Duka lolote linalopendwa sana na wageni pamoja na majumba yenye afisi za kampuni za kigeni yatazua wasiwasi kuhusu usalama uliowekwa baada ya shambulio la West Gate.

Je raia wa Kenya wenye mizizi yao Somalia watashutumiwa?
Kufuatia shambulio hilo, vikosi vya ujasusi pamoja na washirika wao wa magharibi watalazimika kukabiliana na seli za kigaidi nchini.
Huenda kukawa na shinikizo ya kuangazia upya kitengo cha ujasusi ili kujilinda dhidi ya mashambulio mengine katika siku za usoni.
Vikosi vyya usalama vimepongezwa kwa kuchukua hatua mwafaka ikilinganishwa na hatua walizochukua wakati wa shambulio la West Gate ambalo lilitajwa kuwa janga.
Haitarajiwi kwamba kutakuwa na vita dhidi ya Waislamu ama hata dhidi ya raia wa Kisomali kufuatia shambulio hilo.

Hatahivyo mamlaka itakuwa katika shinikizo la kujadiliana na jamii hizo zaidi ili kusaidia katika ujasusi.
Waislamu na raia wa kabila la Somali katika siku zililzopita wamelalamika kuhusu kukandamizwa na kunyanyaswa na vikosi vya usalama.
Wakati huohuo wito wa serikali kuondoa wanajeshi wake Somalia huenda ukaanza tena kutolewa.
 
Al Shabab kwa asilimia kubwa ni Wasomali na wengine wachache wanaowaunga mkono.

Kenya ina raia wenye asili ya Kisomali takriban asilimia 20.

Kwa tunavyowafahamu Wasomali, ni watu wa visasi na hawakubali kuonewa. Ukimuua Msomali leo basi mjukuu wake ataposikia hicho kisa lazima atalipa kisasi. Kama upo hai atakuuwa wewe kama haupo hai atamuuwa mjukuu wako, mradi kisasi kilipwe. Hao ndiyo Wasomali.

Tulishauri humu zamani lakini Wakenya hawatuelewi.

Kinachotakiwa kumaliza hili tatizo ni Wakenya kuita wazee wa Kisomali, wakae nao chini, wakubali kulipa fidia ya damu iliyomwagika Somalia. Wakikubaliana, watachinja na watu kula sadaka pamoja. Yatakuwa yamekwisha. Bila hivyo, hakuna ujanja.

Kenya wanayajua hayo kwani wao si wageni wa Wasomali. Lakini tatizo kubwa ni kuwa vita hii inawaneemesha Wakenya wachache kutoka nchi za magharibi zinazotaka mafuta ya rahisi. Somalia ina mafuta mengi na yapo mpakani na Kenya.

Usishangae kusikia kuwa Kenya imetangaza kugundua mafuta mengi huko mpakani na Somalia baada ya vita hii.

Hii ni vita isiyokuwa na mwisho mwema kwani Wasomali wa ndani ya Kenya usifikiri wao wanaona raha wenzao wanapouliwa na majeshi ya Kenya huko Somalia. Ni hao hao Wasomali wa Kenya wanafanya mashambulizi ndani ya Kenya kulipa kisasi.
 
Labda ungeuliza hivi....jee tukio kama hili lingefanyika Danganyika ingekuwaje......I don't Even wanna imagine
 
Al Shabab kwa asilimia kubwa ni Wasomali na wengine wachache wanaowaunga mkono.

Kenya ina raia wenye asili ya Kisomali takriban asilimia 20.

Kwa tunavyowafahamu Wasomali, ni watu wa visasi na hawakubali kuonewa. Ukimuua Msomali leo basi mjukuu ataposikia hicho kisa lazima atalipa kisasi. Kama upo hai atakuuwa wewe kama haupo hai atamuuwa mjukuu wako, mradi kisasi kilipwe. Hao ndiyo Wasomali.

Tulishauri humu zamani lakini Wakenya hawatuelewi.

Kinachotakiwa kumaliza hili tatizo ni Wakenya kuita wazee wa Kisomali, wakae nao chini, wakubali kulipa fidia ya damu iliyomwagika Somalia. Wakikubaliana, watachinja na watu kula sadaka pamoja. Yatakuwa yamekwisha. Bila hivyo, hakuna ujanja.

Kenya wanayajua hayo kwani wao si wageni wa Wasomali. Lakini tatizo kubwa ni kuwa vita hii inawaneemesha Wakenya wachache kutoka nchi za magharibi zinazotaka mafuta ya rahisi. Somalia ina mafuta mengi na yapo mpakani na Kenya.

Usishangae kusikia kuwa Kenya imetangaza kugundua mafuta mengi huko mpakani na Somalia baada ya vita hii.

Hii ni vita isiyokuwa na mwisho mwema kwani Wasomali wa ndani ya Kenya usifikiri wao wanaona raha wenzao wanapouliwa na majeshi ya Kenya huko Somalia. Ni hao hao Wasomali wa Kenya wanafanya mashambulizi ndani ya Kenya kulipa kisasi.

Is that so easy to bring the carnage to an end!!!!?
 
Tatizo ni kuwa Kenya waliingia vitani huku wakiwa hawajui nini maana ya vita


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Shida kubwa ni uwepo wa raia wakenya wenye asili ya Somalia ndo tatizo na ndowanawaifadhi magaidi swala la kwamba wasomali wana visasi sijui nini Hilo sikubaliani nalo mbona wamepigwa sana na majeshi ya Ethiopia na sidhani kama wamewahi shambulia Ethiopia chamsingi Kenya itoe majeshi somalia ikitoa mambo yatakua safi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 PAC- HIT EM UP
..............."This is how we do it on our side(SOMALIA)
Any of you niggas from New York(KENYA) that want to bring it:
Bring it!
But we(AL SHABAB) ain't singing, we bringing drama"
 
2019118636833686131876400nairobi2.jpg

Hii picha imenitia faraja sana Raia wa kenya bila kujali Dini zao na makabila yao wakisaidiana..cha ajabu Hapa Tanzania,kuna washabiki wa Alshababu mimi nawaita "AlShababu Ugali" kwa maana wakishashiba wanafungua simu zao na kuanza jihadi! Jihadi! Jihadi! Alahu akbar!
 
Back
Top Bottom