Hakikisheni hawa wanachemshwa supu kabisa, hawa hawana haja ya kuwapeleka mahakamani.
Mi siamini mfumo huo wa kupambana na magaidi, Kwa mfano hawa wameshikwa na kikosi spesheli ambacho kimepewa mafunzo ya hali ya juu na wanajua wanachofanya, yani hua hawabahatishi, lakini wale polisi wa kawaida kazi yao kubahatisha, sometimes wanashuku mtu ni gaidi badala ya kuchunguza wanakungojea ukiwa pekyako na kukukamata na hautaonekana tena hata kama walikua hawajapata ushahidi wa kutosha...
Kwenye kupambana na Ugaidi unafaa ujue, Violence leads to more violence, Polisi kuua mtu kwa kumshuku ni gaidi bila kufwata sheria, familia yake, kaka zake, marafiki, jirani, msikiti anapoenda, watu wote hao umewatia chuki na hasira, kilichobaki tu ni sheikh ambaye ana itikadi kali za kidini kuchochea hio jamii kulipiza kisasi au kujiunga na ugaidi.....
Tunafaa tuingize utaalam zaidi ili tuweze kupambana na kesi za kigaidi vizuri zaidi hadi iwe tunaweza kushika mtu, kumshtaki na miezi sita baadae jamaa anahukumiwa..... Baada ya hapo tunaweza hata kutumia ile sheria ambayo haijawahi tekelezwa tangu 1985 ya kunyonga mtu anayehukumiwa kifo..... Mtindo huu wa kufywata sheria ndo utaleta utulivu kwa jamii, lakini mambo ya kuchemsha supu mwishowe tutajipata tunapigana vita vya kidini, Hebu angalia yanayotendeka kule afghanistan, Baada ya marekani kuua zaidi ya Taliban 10,000 ndani ya miaka ishirini, Taliban wa leo ni wengi kuliko wale walioanza vita, Kadri marekani inavyowaua kiholela ndo walikua kaka,dada,jomba na majirani wa alie uliwa wanajiunga na taliban...