Wanabodi,
Tangu kutokea kwa shambulizi kwa Tundu Lissu, ambalo mpaka sasa linaelezewa kufanywa na watu wasiojulikana, kumeibuka shauku kubwa ya kuwabaini hawa watu wanaoitwa kuwa ni watu wasiojulikana huku zikijengwa dhana mbalimbali kuhusiana na wasiojulikana hawa, hadi kufikia kuwanyooshea vidole baadhi ya watu, wakiwemo wale "jamaa" zetu.
Kufuatia taarifa nyingi za watu wasiojulikana kuhusika kwenye baadhi ya matukio na Jeshi letu la polisi ndio mamlaka rasmi ya kufanya uchunguzi na mara zote hutoa taarifa kuhusu kuhusika kwa wasiojulikana ambao mwisho wa siku hubakia hivyo hivyo kuwa wahusika wa tukio fulani ni watu wasiojulikana, kumbe sometimes sii kweli kuwa wahusika ni watu wasiojulikana, sometimes wahusika wa matukio hayo sio watu wasiojulikana bali ni watu 'wasiojulikana'.
Hivyo hili ni bandiko la kuwahusu watu wasiojulikana ambao mwisho wa siku baada ya uchunguzi wa kipolisi, watajulikana, lakini pia kuna mashambulio yanayofanywa na watu 'wasiojulikana', ambao kamwe hawatajulikana!.
Haswa pale ambapo 'wasiojulikana' ni wale "Jamaa Zetu"!.
Hebu fuatilia jinsi " Hawa Jamaa" wanavyotekeleza mashambulizi na mauaji.
1. Kuna kiongozi mmoja mkubwa serikalini anayesemekana alikufa kwa ajali ya gari, ila mwili wake ulikutwa na majeraha ya kitu fulani, inasemekana
ni wale jamaa.
2. Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Mwinyi, Kighoma Malima alipo defect kutoka CCM na kujiunga na NRA, aliugua ghafla na kupoteza maisha. Inasemekana ni wale jamaa.
3. Horace Kolimba akiwa CCM high ranking oficer, aliposema CCM imepoteza Dira na Haina Mwelekeo, alipoteza Marsha kwa kuugua ghafla. Ikasemekana ni "wale jamaa"
4. Kiongozi mwingine mkubwa wa serikali alifariki ghafla kwa ugonjwa baada ya tuu ya kukamilisha ziara ya kutembelea maonyesho ya Saba Saba, mmoja wa hao "jamaa" akajiunga jf na kutueleza kila kitu kuhusu madudu yao humu.
5. Tukio la kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Absolom Kibanda, Roma Mkatoliki, Mwandishi wa habari wa DW, Salma Said, na kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, pia kukihusishwa na "wale Jamaa" wasiojulikana.
6. Tukio la Uvamizi wa Kituo cha TV cha Clouds TV kilichofanywa na DAB, a.k.a PCM, wale makirikiri wenye silaha wanasemekana ni "wale James" na walitumia Nissan Nyeupe!.
7. Yule mpuuzi aliyemnyooshea Nape bastola, anajulikana kwa sura katika media zote, na alikuja kwa kutumia gari Nissan Nyeupe, naye anaelezewa kuwa ni mtu asiyejulikana!. Taarifa za chini chini zinaeleza huyu jamaa ni miongoni mwa "wale jamaa".
8. Huyu Blogger wa Kenya amesema haya kwenye mitandao ya kijamii, hadi akataja majina ya wahusika na magari yaliyohusika ikiwemo hiyo Nissan Nyeupe na sijasikia yoyote akikanusha hata serikali yetu kukanusha.
Hii inapelekea mimi kujiuliza maswali haya.
- Kama wahusika wa Tukio la shambulio la Tundu Lissu, ni "wale jamaa", kwa vile wale ni ma pro, and they have never missed the target, kama ni kweli ni wao, how could they missed the target?. Hawa watakuwa sio wale!, na kama ni wale, saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine!.
- Kama they have 100 ways to do elimination in a good way, natural death, accidents, or any clean job and nobody would've suspected anything, why do such a dirty job?.
- Was Tundu Lissu such a threat to status quo ya yule boss wao?, kama kuna defectors very high rankings wame cross na wamejizolea kura nyingi kuliko zilizomuingiza Kikwete madarakani ile 2010, hawa ndio the real threat!, kwa nini hawa wasiwe targeted?. Why Lissu?.
- What
- Kama kuna chama viongozi wake waliwahi kutuhumiwa kupanga vitendo vya ugaidi na utekaji na video zikaletwa humu, hawawezi kuwa ndio wao waliopanga mpango huo?, kwa kufanya timing ya Dodoma ili wadhaniwe ni "wale jamaa?".
- Kama Wangwe alipotaka kugombea uenyekiti alikufa kwa ajali yenye utata mpaka kesho, na huu ni mwaka wa uchaguzi wa ndani, haiwezekani ika ni friendly fires?.
- Kama Zitto alipotaka kugombea alifanyiwa life atempt kwa sumu, lakini kwa vile ameaga kwao, akasalimika, haiwezekani na Lissu pia ameaga kwao?.
- Kama Mlinzi wa Dr. Alas alishughulikiwa vile, then haiwezekani hii sasa ndio advanced methods za kudeal na the internal threats zao?.
Conclusion Kuwahusu hawa Watu Wasiojulikana acording to the motive behind the shooting.
1. Kama the motive behind shooting ya Lissu ni kwa sababu he is jvery vocal hivyo kuonekana ni mwiba, then hawa wanaoitwa ni wasiojulikana, kiukweli sio watakuwa ni "wale jamaa", kama ni "wale jamaa", then hawa sio watu wasiojulikana, hawa ni watu 'wasiojulikana', kama yule mpuuzi aliyemshikia Nape bastola ni mtu 'asiyejulikana' na mpaka leo hajulikani na kamwe hatajulikana, and if this being the case, then watu hawa hawatajulikana kabisa, hata yule aliyetajwa na blogger wa Kenya, pia ni mtu 'asiyejulikana'. Ila hukumu ya karma itawahusu.
2. Kama the motive wasiojulikana hawa ni partly politics ya siasa za ndani na run of kuelekea 2020, then polisi waendelee na uchunguzi, soon watasalitiana na tutawabaini na watu wa tabaki midomo wazi kwa kutoamini.
3. Lakini kama the motive behind wasiojulikana hawa ni hawa wezi wa rasilimali zetu, na lengo lao ni kutufarakanisha na kutuhamisha kwenye hoja ya rasilimali zetu, ili tusahau makinikia, Tanzanite, Dhahabu, Almasi na Gesi, then, hawa sisi as sisi, hatuna uwezo wa kuwabaini bila msaada wa Scotland Yard, ila, tayari, tumeisha wastukia, hatuta farakana,, tutasimama firm, and under th e united front. Kama lengo ni tufarakane, tukifarakana, tutakuwa tumewapa walichokitaka, tusikubali kufarakana, tushikamane as one
We Wish TL To Get Well Soon.
Paskali