Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

Hizi zote ni hadithi za kufikirika tu. Hadi leo hakuna uthibitisho wa nani hasa alihusika na tukio hilo ovu na la kishetani.

In the long run itajulikana tu, picha zipo za satellite data base!!! ziko very clear, google siku hizi linanasa kila kitu kwa kutumia mitambo ya satalite! Kwa hiyo msiwe na hofu kila kitu kitakuwa hadharani wakati muafaka! Dunia ni ndogo saaaaaaaaaaaaaaaaana mbele ya technologia za sasa!
 
Watajulikana tu hata baada ya miaka 10 'There is no Secrete under the Sun they will confess before God'
 
Mkuu GENTAMYCINE umejaribu kuelezea vizuri kwa muono wako lakini tujaribu kuona kwa upande mwingine basi ukoje.
Ni kweli system ikikuhitaji huwezi kabisa kuchomoka maana inao watu trained wanaojua wana fanya nini.
Lakini system yaweza kutumika Mara mbili, issue official ambayo lazima inapangwa kiuweledi na inafahamika kwa wahusika Wa jambo hilo kwa mkakati kamili na kuna LA pili jambo ambalo halina maslahi ya taifa hivyo linafanyika kiharamu kwa kutumia baadhi ya wahusika Wa system kutekeleza.
Na uharamu huo ndio unao sababisha mambo Ku backfire hadi kuleta sintofahamu ndani ya system hadi wakati mwingine mambo ya "utata" kama yale ya kuhamishianaTabora. Hilo LA siri na haramu ndio laweza kuwa lilitumika kwa Lissu kwa system ile ile kwani Lissu sio tishio kwa taifa na hata ndani ya system anao wafuasi wanaojua umuhimu wake na kumuunga mkono utapangaje kwa uwazi kumdhuru?
Lingine ni ukimya, serikali zote ulimwenguni litokeapo jambo lenye kuichafua ni haraka sana kuweka wazi uchunguzi wake kujisafisha. Lakini mbona hii imeufunga uchunguzi pamoja na mambo ya wazi kabisa ikiwamo kuondelewa ulinzi, CCTV camera na mengineyo?
Kubaki na kusema dereva dereva ni argument isiyo na mashiko hata kidogo katika issue iliyochafua nchi kwa kiasi kikubwa. Tukubaliane tuu kuwa serikali imeshafunga siku nyingi file LA Lissu kwani majibu inayajua na kama ni kwavile ni inside job basi ni wazi serikali hii haitufai hata kwa dakika moja. Inashindwa kichukua hatua? Yaani mie nikimuua mke wangu watasema hayo ni mambo yetu ya ndani?
Mkuu Chakaza, nisome hapa taratibu, niliwahi kuzungumzia hili.
Conclusion Kuwahusu hawa Watu Wasiojulikana na 'wasiojulikana', according to the motive behind the shooting.
1. Kama the motive behind the shooting ya Lissu ni kwa sababu he is jvery vocal hivyo kuonekana ni mwiba, then hawa wanaoitwa ni wasiojulikana, kiukweli sio wasiojulikana, hawa watakuwa ni 'wasiojulikana' ambao ni wale "jamaa zetu", kama ni wale "jamaa zetu", then hawa sio watu wasiojulikana, hawa ni watu 'wasiojulikana', kama yule mpuuzi aliyemshikia Nape bastola ni mtu 'asiyejulikana' na mpaka leo hajulikani na kamwe hatajulikana, and if this being the case, then watu hawa hawatajulikana kabisa, hata yule aliyetajwa na blogger wa Kenya, pia ni mtu 'asiyejulikana'. Ila hukumu ya karma itawahusu wahusika wote.

2. Kama the motive behind the shooting ya wasiojulikana hawa ni partly politics ya siasa za ndani na run of kuelekea 2020, then polisi wetu waendelee na uchunguzi, soon watasalitiana na tutawabaini na watu wa tabaki midomo wazi kwa kutoamini.

3. Lakini kama the motive behind wasiojulikana hawa ni hawa wezi wa rasilimali zetu na lengo lao ni kutufarakanisha sisi na serikali yetu kwa kutuhamisha kwenye hoja ya rasilimali zetu, ili tusahau makinikia, Tanzanite, Dhahabu, Almasi na Gesi, then, hawa, sisi as sisi, hatuna uwezo wa kuwabaini bila msaada wa Scotland Yard, ila, kwa vile tayari, tumeisha wastukia nia yao ovu, hatuta farakana, tutasimama firm as one, and under th e united front. Kama lengo ni ili tufarakane, tuichukie serikali yetu kuwa ni ya kidikiteta, na kuanza kufanya vurugu, tukifarakana, tutakuwa tumewapa walichokitaka, tusikubali kufarakana, kwa kufakaranishwa na wafakaranishaji hawa, lets stand together as one, tupendane, tuheshimiane, tuvumiliane, tustahimiliane, tubishane bila kupigana, tukubaliane kwenye maslahi ya taifa na ikishindikana tukashindwa kukubaliana, then tukubaliane kutokubaliana lakini mwisho wa siku, wasiojulikana wajulikane lakini 'wasiojulikana', sijui.

I'm not very certain kuhusu majaaliwa ya position ya Mwigulu, but lets keep on, wishing TL, To Get Well Soon!.

Paskali
P.
 
Naona umewataja taja mara nyingi watu wasiojulikana hadi wamejulikana.
Kisanduku ndiyo alikwenda Dodoma na Nissan nyeupe ile gari ya nyuma alikuwemo Le mutuz na wenzake ambao walitoa Amri ya papara kwa mpiga Risasi, akapiga kwa papara huku wakisepa faster wasijulikane, wakiletwa FBI wakawahoji hao wawili watapata jawabu pasipo hata kufika Eneo la Tukio lenyewe.
 
Hii issue ya hawa wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu, bado inasumbua.
P
Wanajulikana sana kwa sasa ingawa ni vigumu kuwakamata kutokana na kulindwa na wale waliowatuma kule Dodoma na wengine sasa wamehamia kwa waganga wa kienyeji baada ya kusikia Lisu anakaribia kurejea nchini hivi karibuni.
 
Wanabodi,
Tangu kutokea kwa shambulizi kwa Mhe.Tundu Lissu, ambalo mpaka sasa linaelezwa kufanywa na watu wasiojulikana, kumeibuka shauku kubwa ya watu kutaka kuwabaini hawa watu wanaoitwa kuwa ni watu wasiojulikana, ni kina nani, wanatumwa na nani na lengo lao ni ninri, kunakopelekea kujengwa kwa dhana mbalimbali kuhusiana na wasiojulikana hawa, hadi kufikia kuwanyooshea vidole baadhi ya watu, wakiwemo wale "jamaa" zetu kuwa ndio 'wasiojulilana' hawa!.

Ukimya wa Jeshi letu la polisi kwa matukio haya, na ushahidi wa wazi upo lakini hakuna any update ya uchunguzi, na utulivu wa Comred Mwingulu Nchemba, kuonyeshea, he knows something kinyume cha dhamira yake, kujiuzulu awamu hii ni suicide, hivyo yupo yupo tuu na kimya hiki kitampelekea ama kutumbuliwa ama kubadilishwa na kuwekwa mtu ambaye ana uwezo wa kusema uongo na mchana kweupe na macho makavu ili kuitetea serikali kila inapo mess. Kwa vile Mwigulu ni mtu wa haki, ameamua kuliko kutenda dhambi ya kusema uongo, ameamua bora ajinyamazie tuu kusubiria liwalo na liwe kwenye hatima yake!, time will tell!.

Kufuatia taarifa nyingi za watu wasiojulikana kuhusika kwenye baadhi ya matukio na Jeshi letu la polisi ndio mamlaka rasmi ya uchunguzi nchini Tanzania (nchi za wenzetu wanazo private investigators, mamlaka rasmi ikishindwa, unaajiri private investigator, uchunguzi unafanywa), na mara zote jeshi letu la polisi hutoa taarifa kuhusu kuhusika kwa watu wasiojulikana ambao mwisho wa siku hubakia hivyo hivyo kuwa wahusika wa tukio fulani ni watu wasiojulikana, ambao hawajajulikana mpaka mwisho!.

Kumbe sometimes sii kweli kuwa wahusika wa basdhi ya matukio fulani ni watu wasiojulikana, sometimes wahusika wa matukio hayo sio watu wasiojulikana bali ni watu 'wasiojulikana'!.

Hivyo hili ni bandiko fikirishi tuu la dhana ya kuwahusu watu wasiojulikana ambao mwisho wa siku baada ya uchunguzi wa kipolisi, watakuja kujulikana, lakini pia kuna mashambulio yanayofanywa na watu 'wasiojulikana', ambao hawa, kamwe hawakuja kujulikana!, haswa pale ambapo 'wasiojulikana' hawa ni wale "Jamaa Zetu"!.

Hebu fuatilia jinsi hawa ,"Jamaa Zetu" 'wasiojulikana', wanavyotekeleza mashambulizi mbalimbali na sometimes hadi elimination in a very professional way by doing a good clean job hivyo kamwe hawawezi kuja kujulikana, hivyo kubaki ni watu 'wasiojulikana', daima dumu!.

Hii hapa chini ni mifano tuu ya baadhi ya dhana hizo, na sio lazima iwe ni kweli, ila haya matukio ni matukio ya kweli yaliyotokea, sio lazima yawe yalitekelezwa na 'wasiojulikana', yanawezekana yalitokea tuu naturally ila kwa vile kulikuwa na dhana zilizosemwa, mimi nayataja tuu na links ya hizo dhana, ili ufikie conclusion wewe mwenyewe na sio kulishwa hitimisho.

1. Kuna kiongozi mmoja mkubwa serikalini anayesemekana alikufa kwa ajali ya gari, ila mwili wake ulikutwa na majeraha ya kitu fulani, inasemekana ni wale "jamaazetu"
Kifo cha Sokoine: Tujiondoe jela ya kifikra | JamiiForums | The ...

2. Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Mwinyi, Kighoma Malima alipo defect kutoka CCM na kujiunga na NRA, aliugua ghafla na kupoteza maisha. Inasemekana ni wale "jamaa zeta".
Ukweli wa kifo cha Kighoma Ally Malima ni upi? | JamiiForums | The ...

3. Horace Kolimba akiwa CCM high ranking oficer, aliposema CCM imepoteza Dira na Haina Mwelekeo, alipoteza maisha kwa kuugua ghafla. Ikasemekana niwale "jamaa zetu"
Kabla ya kutoka ccm jiulize mara mbili;horace kolimba,gen kombe ...
Wananchi wakitaka kujua nani alimuua nani? | JamiiForums | The ...
Vifo vya viongozi vyenye utata | JamiiForums | The Home of Great ...

4. Kiongozi mwingine mkubwa wa serikali alifariki ghafla baada ya tuu ya kukamilisha ziara ya kutembelea maonyesho ya Saba Saba, mmoja wa hao "jamaa" akajiunga jf na kutueleza kila kitu kuhusu madudu yao humu na kutueleza humu hiyo ni kazi, ya wale "jamaa zetu".
Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa ...
5. Tukio la kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Absolom Kibanda, Roma Mkatoliki, Mwandishi wa habari wa DW, Salma Said, na kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, pia kukihusishwa na wale "Jamaa zetu" 'wasiojulikana'.

6. Tukio la Uvamizi wa Kituo cha TV cha Clouds TV kilichofanywa na wale makirikiri wenye silaha wanasemekana ni wale ""jamaa zetu" na walitumia Nissan Patrol Nyeupe!.

7. Yule mpuuzi aliyemnyooshea Nape bastola, anajulikana kwa sura katika media zote, na alikuja kwa kutumia gari aina ya Nissan Patrol Nyeupe, naye licha ya picha yake na sura yake kuenea kote kuanzia kwenye mainstream media hadi kwenye social media, lakini na yeye a anaelezewa kuwa ni mtu 'asiyejulikana'!. Taarifa za chini chini zinaeleza huyu jamaa ni miongoni mwa wale jamaa "jamaa zetu".

8. Huyu Blogger wa Kenya amesema haya kwenye mitandao ya kijamii, Blogger Robert Alai(Kenya) atoa siri ya waliompiga Lissu risasi. Amtaja RC Makonda...

hadi akataja majina ya wahusika na magari yaliyohusika ikiwemo hiyo Nissan Patrol Nyeupe na sijasikia yoyote akikanusha taarifa ya blogger huyu!, hata serikali yetu kukanusha. Hivyo sometimes silence ni admission of guilt, kwa vile ni 'wasiojulikana', hawana sababu ya kujibu lolote wasije wakajulikana!.
Hii inapelekea mimi kujiuliza maswali haya.
  1. Kama wahusika wa Tukio la shambulio la Mhe. Tundu Lissu, ni wale "jamaa zetu", kwa vile wale ni ma pro, they have one million ways to do things, in a good clean and professional way.and they have never missed a target!, sasa kama kweli ni wao, ndio waliomshambulia Lissu, how could they do such a dirty job?!, how could they missed a target in such close range, hadi watumie risasi 38!, wakati kwa trained snipers, only one is enough?!.
  2. Tuambiane ukweli jamani, hawa waliofanya haya watakuwa sio wale 'jamaa zetu!' na kama ni kweli walikuwa wale, saa hizi si tungekuwa tunazungumza mengine!. Unless kama kweli ni wao, ila wamejifanya to miss the target makusudically ili ku dupe the public kwa kupotezea maboya kwa kupoteza lengo ionekane waliofanya tukio lile sio ma pro ili tukio lionekane limefanywa na amateurs!.
  3. Kama they have 100 ways to do elimination in a good clean professional way by doing a clean job, on natural death look like, accidents, or any clean job that nobody would've suspected anything, why did they do such a bad dirty job?!.
  4. Hawa " jamaa zetu" hufanya elimination kwenye some serious threats to our national security, or threats to the status quo iliyopo, swali la kujiuliza ni since ya the ruling class, sasa when was Mhe.Tundu Lissu, has ever been such a threat to warrant such elimination?!. Kama kuna defectors very high rankings wame cross na wamejizolea kura nyingi kuliko zilizomuingiza Kikwete madarakani ile 2010, hawa ndio the real threats!, hivyo issue ingekuwa ni eliminations of status quo threats, kwa nini hawa ambao ndio the real threats wasiwe targeted?, aje kuwa targeted Lissu?!. Why Lissu?!.
  5. What if kilichomtokea Lissu ni kutokana na issue nyingine yoyote na sio siasa?. Hili niliwahi kushauri humu JamiiForums
  6. Kama kuna chama viongozi wake waliwahi kutuhumiwa kupanga vitendo vya ugaidi na utekaji na video zikaletwa humu, hawawezi kuwa ndio wao waliopanga mpango huo?, kwa kufanya timing ya Dodoma ili wadhaniwe ni "wale jamaa zetu?".
  7. Kama Wangwe alipotaka kugombea uenyekiti alikufa kwa ajali yenye utata mpaka kesho, na huu ni mwaka wa uchaguzi wa ndani, haiwezekani ikawa ni inside job ya friendly fires?.
  8. Kama Zitto alipotaka kugombea alifanyiwa life atempt kwa sumu, lakini kwa vile ameaga kwao, akasalimika, haiwezekani na Lissu pia kwao ameaga na ndio maana amesalimika?.
  9. Kama Mlinzi wa Dr. Slaa, aliaminika sana, lakini alipostukiwa, alishughulikiwa ipasavyo!. Haiwekani dereva wa Lissu has a hand?!.
  10. Maadam Chadema wanao utaratibu wao wa ndani wa kuwashughulikia watu ambao threats kwao. Jee haiwezekani tukio la Lissu linaweza kuwa ni inside job? na alihudumiwa hivyo na watu wao? ndio maana dereva hakuguswa?!. Kama watu wanaoweza kushughulikia hivi binadamu wenzao, they are capable of doing anything, then haiwezekani hii sasa ndio the advanced methods za kudeal na the internal threats zao?.
Conclusion Kuwahusu hawa Watu Wasiojulikana na 'wasiojulikana', according to the motive behind the shooting.
1. Kama the motive behind the shooting ya Lissu ni kwa sababu he is jvery vocal hivyo kuonekana ni mwiba, then hawa wanaoitwa ni wasiojulikana, kiukweli sio wasiojulikana, hawa watakuwa ni 'wasiojulikana' ambao ni wale "jamaa zetu", kama ni wale "jamaa zetu", then hawa sio watu wasiojulikana, hawa ni watu 'wasiojulikana', kama yule mpuuzi aliyemshikia Nape bastola ni mtu 'asiyejulikana' na mpaka leo hajulikani na kamwe hatajulikana, and if this being the case, then watu hawa hawatajulikana kabisa, hata yule aliyetajwa na blogger wa Kenya, pia ni mtu 'asiyejulikana'. Ila hukumu ya karma itawahusu wahusika wote.

2. Kama the motive behind the shooting ya wasiojulikana hawa ni partly politics ya siasa za ndani na run of kuelekea 2020, then polisi wetu waendelee na uchunguzi, soon watasalitiana na tutawabaini na watu wa tabaki midomo wazi kwa kutoamini.

3. Lakini kama the motive behind wasiojulikana hawa ni hawa wezi wa rasilimali zetu na lengo lao ni kutufarakanisha sisi na serikali yetu kwa kutuhamisha kwenye hoja ya rasilimali zetu, ili tusahau makinikia, Tanzanite, Dhahabu, Almasi na Gesi, then, hawa, sisi as sisi, hatuna uwezo wa kuwabaini bila msaada wa Scotland Yard, ila, kwa vile tayari, tumeisha wastukia nia yao ovu, hatuta farakana, tutasimama firm as one, and under th e united front. Kama lengo ni ili tufarakane, tuichukie serikali yetu kuwa ni ya kidikiteta, na kuanza kufanya vurugu, tukifarakana, tutakuwa tumewapa walichokitaka, tusikubali kufarakana, kwa kufakaranishwa na wafakaranishaji hawa, lets stand together as one, tupendane, tuheshimiane, tuvumiliane, tustahimiliane, tubishane bila kupigana, tukubaliane kwenye maslahi ya taifa na ikishindikana tukashindwa kukubaliana, then tukubaliane kutokubaliana lakini mwisho wa siku, wasiojulikana wajulikane lakini 'wasiojulikana', sijui.

I'm not very certain kuhusu majaaliwa ya position ya Mwigulu, but lets keep on, wishing TL, To Get Well Soon!.

Paskali
Naomba nikapumzike!!
 
Hivi zile cctv nazo kuondolewa bado mtu unaweza kusema hili tukio lilifanywa na watu wa ndani ya cdm. ?
 
Naona mipasho na porojo za vibarazani uswahilini tu.Waliofanya tukio hilo wanajulikana na ndio hao walioondoa CCTV eneo la tukio na ndio hao waliohakikisha kuwa walinzi wrote wanaondolewa siku hiyo
 
Kuhusu Zitto kupewa sumu, mimi nawalaumu waandishi wetu wa habari na akili zao fupi kama mkia wa nguruwe. Zitto aliugua akiwa ktk kikao cha chama bagamoyo kama sikosei. Akaugua tumbo akalazwa agha Khan. Taarifa ya madaktari ikasema tatizo la Zitto ni 'food poisoning'.

Makanjanja wetu walivyoona neno poisoning wakajua maana yake amepewa sumu. Kimsingi food poisoning ni kuchafuka kwa tumbo. Kunatokea ukila chakula kichafu au ukila chakula halafu kikachacha tumboni kutokana na kuchelewa kumeng'enywa. Ni mwendo wa kuhara. Ni nan hajawahi kuchafuka tumbo?

Kitu cha kusikitisha tafsiri ya kupewa sumu ilitolewa na gazeti la Mwananchi ukurasa wa kwanza, gazeti kubwa kuliko yote Tanzania kwa market share. Sishangai mkuu Pasco kuendeleza hii stori inayotokana na tafsiri ya uongo ya food poisoning. Wangekuwa na akili hawa waandishi wetu wangeuliza aina ya sumu (chemical composition) aliyopewa. Zitto nae alivyo mjanja na Mafia wa siasa akaitumia fursa hizo kupata sympathy approval.

Kama chadema ina historia ya kuua viongozi wake basi wachunguzwe, washtakiwe na wafungwe. La sivyo ni propaganda tu.

"Wangekuwa na akili hawa waandishi wetu wangeuliza aina ya sumu (chemical composition) aliyopewa".

Wasingeweza kuhoji kwa sababu ya ukanjanja wao.
 
Naona mipasho na porojo za vibarazani uswahilini tu.Waliofanya tukio hilo wanajulikana na ndio hao walioondoa CCTV eneo la tukio na ndio hao waliohakikisha kuwa walinzi wrote wanaondolewa siku hiyo
Walinzi wa Getini na aliyekuwa akiangalia cctv hawajawahi kuhojiwa ni ajabu ya Duniani kote, cha kushangaza wamekalia kusema wanamtaka dereva wa Lisu ili waende kumtesa au wafanye vyovyote apate kuleta uzushi mwingine wakwepe lawaza dhidi yao, aliyewatoa walinzi ama kuwazuia kukabiliana na tukio ni mmojawapo wa wapanga njama hizo.
 
"Wangekuwa na akili hawa waandishi wetu wangeuliza aina ya sumu (chemical composition) aliyopewa".

Wasingeweza kuhoji kwa sababu ya ukanjanja wao.
Pia wahoji CCTV za kule Dodoma zipo wapi? na ni kwa nini Ziliondolewa? na nina alitoa amri ya kuziondoa? na pia ni kwa nini walinzi wa Getini waliacha Geti wazi na kujificha pasipo kujihami wakati walikuwa na bunduki? Wakiletwa FBI au Scotland’ yard ni mda mchache watautumia kutoa jawabu la kila kitu,
 
Back
Top Bottom