Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Watoto saba wamekufa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulizi la angani nchini Niger hii ikiwa ni kulingana na gavana wa jimbo moja nchini humo
Shambulizi hilo lililofanywa na vikosi vya Nigeria katika eneo la mpakani lilikuwa likiwalenga majambazi lakini badala yake liliwaua na kuwajeruhi watoto hao siku ya Ijumaa
Kulingana na Gavana Chaibou Aboubacar wa mkoa wa Maradi jeshi la Nigeria lilikuwa likiwalenga majambazi hao, lakini kwa bahati mbaya liliwakuta watoto hao waliokuwa katika kijiji la Nachade.
DW Swahili